Buriani rafiki na ndugu yangu Salum ''Slim'' Shamte (1951 - 2020)

Buriani rafiki na ndugu yangu Salum ''Slim'' Shamte (1951 - 2020)

BURIANI RAFIKI NA NDUGU YANGU SALUM ''SLIM'' SHAMTE 1951 - 2020

Nimeingia maktaba yangu ya picha ndani ya photo album natafuta picha moja ya Slim niliyompiga kiasi cha miaka 20 iliyopita mwezi mtukufu wa Ramadhani kwenye futari ambayo kila mwaka alikuwa akitualika nyumbani kwake Bombo.

Kwa kipindi chote nilichoishi Tanga kila Ramadhani kulikuwa na siku Shamte anatualike tunajumuika nyumbani kwake kufuturu pamoja.

Tunaanza kwa kufungua muazini kwa maji, juisi na tende kisha tunasali kwenye bustani yake na baada ya hapo tunafuturu tukimaliza tunaomba dua na kutawanyika.

Futari ya Slim Shamte nyumbani kwake Bombo, Tanga nzima tukiipenda si kwa ajili ya mapochopocho bali futari hii ilikuwa inaukusanya mji mzima wa Tanga nyumbani kwa Shamte.

Slim alikuwa akiwaalika wengi katika jamii ya Tanga

Mamudir yaani wakuu wa vyuo vyote vya Tanga na masheikh wa mji walikuwa wanahudhuria futari hii na utawaona wamekaa pamoja bega kwa bega na raha inakuja pale panapokimiwa ili tusali.

Hapo katika hadhira ile wapo wanazuoni wa juu kabisa katika Afrika ya Mashariki lakini kila mmoja inapokuja kuongoza sala ile ya Maghrib atajirudisha nyuma kutaka mwenzake atangulie.

Tanga ni kati ya miji michache sana katika Afrika ya Mashariki ambayo hawezi mtu kutoka nje akaenda pale kwa nia ya kusomesha.

Allah ameijalia Tanga kuwa mji ambao unajitosheleza kwa elimu ya dini kiasi wanafunzi wanatoka nje ya Tanga kuja pale kusoma iwe TAMTA, Zaharua, Maawa au Shamsi Maarif.

Pale tuliposimama kusubiri ikama ili tuswali Maghrib katika safa hii ya wasomi wapo vijana na wapo wazee na hawa wazee wengine ni walimu waliowasomesha hawa wanazuoni vijana.

Hapa wanazuoni vijana wanajua wazi kuwa kusalisha sala ile basi aula zaidi ni mwalimu wao, kwanza kwa ule ualimu wa kuwasomesha wao anastahili yeye kuwasalisha na pili haiyumkini kuwa mwalimu aongozwe na wamanafunzi wake.

Basi utasikia sheikh anasema, ''Nyote mwakimbia kusalisha hoja yenu ati atangulie mzee sasa mtafanza haya hadi lini? Sasa mswalishe nasi tu hai tukuoneni kama kweli mwapatia.''

Watu wa Tanga ni watu fasaha sana wanapozungumza utapenda kusikiliza.

Sheikh atasema haya maneno kwa maskhara kwa ile lafidh ya Kitanga lakini hatatangulia atamwita mmoja wa vijana wanazuoni kuja kusalisha.

Hapa inakuwa ile itifaki na adabu ya elimu imezingatiwa.

Hii ishakuwa amri na kijana atasogea mbele na kusalisha.

Kuanzia hapa sasa tunapata raha nyingine kwa kusikiliza kile kiraa, yaani usomaji wa Qur'an kwa mazingatio ya hukumu zake zote.

Naam na imam sharti asome vizuri eti kwani nyuma yake anasalisha pamoja na sisi maamuma wenzangu mie, wanazuoni wakubwa.

Siku zote kila mwaka ilikuwa inapofika kipande hiki cha umma kusali pamoja pale nyumbani kwa Shamte kwenye bustani yake yenye maua mazuri nafsi yangu ilikuwa inaburudika sana.

Nitapenda kueleza jambo hapa.

Pamoja na maua mazuri haya na majani, Slim nyumbani kwake kapanda mkonge kuzunguka wigo mzima bila shaka kuufahamisha ulimwengu kuwa yeye ni mtu wa mkonge.

Nimesema kuwa nilikuwa natafuta picha moja ya Slim niliyompiga zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Bahati mbaya sana kwangu picha hii sikuipata.

Nitaeleza kwa nini picha hii mimi nilitaka niiweke hapa muione.

Abdallah Mgambo amemtangulia Salum Shamte kwa siku moja kufariki.

Picha hii yupo Abdallah Mgambo na Slim nimewapiga mwezi wa Ramadhani Mkonge Hotel kwenye futari ya Shamte.

Iweje kiwanja tumebadili hatufuturu nyumbani tumehamia Mkonge Hotel, moja ya hotel za kupendeza mjini Tanga?

Siku ile mvua kubwa ilinyesha kuanzia asubuhi.

Mimi nikiishi si mbali na nyumbani kwake Shamte na mkewe Bi. Mariam.

Nikampigia simu Slim kumuuliza itakuwaje futari na mvua ile nikitambua fika kuwa ndani ya nyumba yake tusingeweza kuenea hata kidogo lau kama nyumba yake haikuwa kibanda.

Slim akanijibu kwa namna yake ambayo marafiki zake tukijua, anazungumza huku anacheka, ''Sidney tutafuturu In Shaa Allah.''

Sikupata kumuona Slim kaweka uso wa jiwe hata siku moja yeye saa zote ni mtu wa tabasamu.

Futari ya mwaka ule tulifuturu Mkonge Hotel na kwa hakika mwaka ule Shamte alitustarehesha juu ya kuwa baadhi yetu tulilowa.

Hapa Mkonge Hotel siku ile nilipiga picha nyingi katika hali ya mvua ile na wingu lile.

Abdallah Mgambo ambae kama nilivyoelza awali kuwa alimtangulia Shamte kufariki kwa siku moja alikuwa amenitembelea nikamwambia kuwa kaja na mguu mzuri kwani siku ile tutafuturu kwa Shamte.

Abdallah Mgambo na Shamte wote niliwanasa katika camera yangu.

Nimesikitika sana kutoiona picha hii kwani kwangu ni kumbukumbu nzuri sana.

Shamte alikuwa akikualikeni futari yeye hali kwa utulivu muda wote anatoa maelekezo au kachukua hiki mwenyewe kampelekea yule mara wameingia wageni wamechelewa ataelekeza wawekwe wapi kukaa na nani akae na nani nk. nk.

Chakula kinashuka vizuri ikiwa unakula pamoja na marafiki zako.

Shamte alikuwa na rafiki yake kipenzi Sheikh Balhassan.

Sheikh Balhassan alikuwa miongoni mwa masheikh wanaoheshimika sana pale mjini.

Kila mwaka baada ya kufuturu Shamte atamuomba Sheikh Balhassan aombe dua.

Sayyid Muhammad Hashim kutoka Tanga kabla ya maziko aliposimama kutoa rambirambi alisema kuwa watu wa Tanga wamejiinamia kwa majonzi kama tulivyoijiinamia sisi watu Dar es Salaam pale nyumbani kwa Shamte, Mbweni.

Hakuna madrasa Tanga ambayo Shamte hakupata kuinyooshea mkono.

Hujapata wewe kumuona mtu karim kama Shamte.

Slim alikuwa mtu karim mlango wa nyumba yake ulikuwa wazi kwa kila muhitaji na hakujua kumnyanyapaa mtu.

Hakuna ambae mbae alikuwa hamjui Shamte Tanga kuanzia mjini hadi vijijini achilia vile vijiji ambavyo kuna mashamba ya mkonge.

Nimepata kuwa na ''great moments,'' na Shamte nyingi tu baadhi za kuchekesha na nyingine za kuogofya na kusikitisha.

Huenda wengine wasifahamu yale ya ndani ambayo Shamte alipata kukutananayo akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Katani Limited.

Mti wenye matunda ndiyo unaopopolewa.

Kuna walioona katika viongozi kuwa wana haki zaidi ya Shamte ya kutia vidole vyao katika yale aliyokuwanayo Slim na wanaona hiyo ni haki yao kwa sababu ya nafasi zao.

Zaidi ya miaka 20 iliyopita katika mazungumzo alipata kunihadithia dhiki alizokuwa anapata kutoka kwa kiongozi mmoja aliyedhani kuwa yeye yuko juu ya kila mtu katika mkoa ule.

Shamte alikuwa akimstahamilia na kufanya staha kwa kuheshimu ule umri wa huyu bwana.

Slim alishukuru bwana yule alipoondoka Tanga.

Naamini pale nyumbani kwake Mbweni kabla ya maziko ulipokuwa unasomwa wasifu wake wengi walistaajabishwa na yale ambayo Shamte aliyafanya katika umri wake katika biashara na ujasiriamali.

Neno hili, ''ujasiriamali,'' mimi kwa mara ya kwanza nililisikia kutoka kwa Shamte.

Nimebahatika pia kuwepo kwenye shughuli zake nyingi kuanzia mkutano ya kimataifa kuhusu mkonge uliofanyika Tanga, uzinduzi wa bidhaa mpya aliofanya Golden Tulip, Dar es Salaam kwa kutaja machache.

Lakini katika miradi hii yote hakuna mradi ulionivutia kama mradi wa Hale wa kufua umeme kutoka kwenye gesi.

Kila siku akinisisitizia niende kuutazama.

Nilifika Hale na nilishangazwa kuona jinsi makapi ya mkonge yalivyokuwa yakitoa gesi iliyogeuzwa kuwa umeme na umeme ule ukawasha ukatumika kiwandani na katika nyumba za jirani.

Msomaji wa wasifu wa Shamte alisahau kitu kimoja kuwaeleza waombolezaji.

Salum Shamte alikuwa ''super intelligent.''

Mtihani wa Cambridge ''O'' Level alipata credit 9 ndani yake sijui ziko ''Distinction,'' ngapi.

Nini maana yake kupasi namna hii?

Maana yake Shamte angeliweza kusoma chochote na narudia chochote katika mgongo huu wa ardhi.

Pasi hizi ndizo zilizomuingiza Chuo Kikuu cha Nairobi.
Lakini kuna wengi sana ambao haya wala hawakuyajua walimtazama Shamte kama Mswahili mmoja,

Ramadhani Madabida alisimama kuzungumza kwa niaba ya familia ya Shamte.

Hakuweza kuzungumza aliishia kutoa salamu na kumswalia Mtume akaangua kilio cha kwiki na ilibidi aondolewe akakae chini apumzike.

Vipi Madabida ataweza kumzungumza mpenzi wake, rafiki yake ndugu yake, shemeji yake aliyemuoza dada yake Bi. Zarina bint Juma na kupata watoto wema mmoja wa kiume Abdulwahab Madabida yeye pale aliposimama kuzungumza anamuona Abdulwahab akipita akishughulika katika msiba wa mjomba wake?

Vipi utamtegemea Madabida aweze kueleza kote alimopita na Slim kuanzia Pugu Sekondari wakiwa vijana wadogo hadi alipomuoa dada ya rafiki yake kipenzi?

Madabida alitueleza yote ya hisani baina yao katika lile chozi lake.

Haya ni katika yale ambayo watengenezaji filamu kama David Lean hutengeneza senema zinazoitwa, ''Block Blaster.''

Sayyid Muhammad Hashim aliwaambia watu wa Dar es Salaam kuwa, ''Nyinyi mnamjua Shamte kwa mambo ya mkonge, sisi Tanga tunamjua Shamte kama kiongozi wa dini.''

Tunakuomba Mola wetu Wewe uliye Hakim Muadilifu muamulie ndugu yetu Shamte kwa haki katika yale yaliyomsibu katika siku zake za mwisho hapa duniani.

Amin

PICHA:

View attachment 1405601
Slim wa kwanza kulia Mohamed Said, Mohamed Bhinda, Salum Matimbwa, Abdallah Tambaza na Abdallah Shamte mazikoni makaburi ya Msasani Februari 2020.

View attachment 1405608
Sheikh Balhassan siku ya harusi ya mtoto wa Shamte, Juma ambaye ni huyo wa kwanza kulia.

View attachment 1405612
Salum Shamte ni huyo wa tatu kushoto na wa kwanza ni Sayyid Muhammad Hashim hapo ni harusini Tanga miaka mingi iliyopita.
Kwa nini aliitwa Slim, na ilimaanisha nini?
 
Kwa nini aliitwa Slim, na ilimaanisha nini?
Jidu...
Tulipokuwa watoto tuko shule kila mtu alikuwa na ''nickname'' yake.''

Majina tu wala hayakuwa na maana yoyote.

Kulikuwa na Mazola, Kirk Douglas, Marlon Brando, Yongo, Livingstone Madegwa,
Kitonsa na mengine mengi majina ya wacheza mpira Ulaya na waigizaji wakubwa kutoka Hollywood.
 
Jidu...
Tulipokuwa watoto tuko shuele kila mtu aliuwa na ''nickname'' yake.''
Majina tu wala hayakuwa na maana yoyote.

Kulikuwa na Mazola, Kirk Douglas, Marlon Brando, Yongo, Livingstone Madegwa,
Kitonsa na mengine mengi majina ya wachaza mpira na waigizaji wakubwa kutoka Hollywood.
Asante kwa jibu lako ingawaje linakwepa my follow up question.
Mimi vile vile najua hayo yote maana ni mtoto wa DSM.
Marijani Shaaban tutulisoma wote Tambaza.
Nakujua ndugu yangu MSA, wewe ni mtetezi wa wazee wako wa mwambao ambao ni waislamu.
Sasa huyu "Slim" kujitukuza kwa jina, nickname ya kiingereza, hapo naina unapiga ngima kwenye maji.
 
Huyu ndugu yangu ni marehemu.

Sote sisi tulikuwa na majina ya kupanga na wala hayakuwa na uhusiano wowote na dini au kujitukuza kwa aina yoyote ile.

Majina niliyotaja hapa wengi tukiitana hivyo pale Saigon Club miaka ya 1967 wengi wako shule za msingi ni watoto wadogo.

Tukienda senema Empire kuangalia ''Westerns'' tukimuona muigizaji umempenda unachukua jina lake.

Hayakuwa mambo wanayofanya watu wazima.

Wengi wenu ambao pengine hamkutujua sisi makuzi yetu nimeona mnababaishwa na mengi.

Wasichana wa wakati wetu walikuwa wakijipa majina ya wacheza senama wa kike kama Ann Magret, Ursulla Andress, Nancy Sinatra.

Hizo zilikuwa nyakati nyingine kabisa Waingereza waliziita ''The Roaring 60s.''

Katika safari zangu nje nimewashangaza wengi wanaponialika majumbani kwao nakuta ala za muziki kama piano, guitar nk.

Basi hupiga piano ingawa niko ''rusty,'' kwa kukosa kupiga kwa muda mrefu na hushangaa wakaniuliza wapi nilijifunza.

Hizi ni ''taste'' mtu anazipata kutokana na makuzi.

Nina ufahamu mkubwa sana wa jazz.

Hapo chini niko nyumbani kwa rafiki yangu Dr. Harith Ghassany Muscat nilikuwa nampigia nyimbo tena ni hymn, ''Crying in the Chapel.''

Hii nyimbo ya kanisani iipata umaarufu baada ya kupigwa na Elvis Presley ambae alikuwa ''idol'' wangu katika ''teens.''

Yeye na mkewe walishtuka sana wakaniuliza wapi nimejifunza.
Ikiwa umesoma na Marijani basi wewe ni mdogo sana kwangu.

Namfahamu Marijani toka utoto Gerezani yeye na Yusuf Kaungu wote ni marehemu Allah awalaze pema peponi.

Wote walikuwa wachezaji mpira hodari sana.

Marijani alikuwa mlinda mlango wa Kahe Republic na Kaungu alicheza Simba.

Sikwepi swali wakati mwingine nakaa kimya kwa kuwa panakuwa hapana haja ya kufanya ubishani.

Mimi hupenda kueleza yake ambayo watu hawayajui.

Hii ina tija zaidi.

Mimi sijatetea wazee wangu bali nimeiandika historia ya wazee wangu vipi walipambana na ukoloni wa Muingereza kwa kuasisi vyama vilivyokuja kuwaunganisha watu wakawa wamoja wakapigania uhuru wakiwa wameshikana kama taifa.

Waliunda African Association 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 na TANU 1954.

Hii ni historia iliyokuwa katika hatari kubwa ya kupotea.

Huku si kutetea.

1661634546401.png

1661635610288.png

Humburg nyumbani kwa Abdilatif Abdalla.
 
View attachment 2336890
View attachment 2336898

Humburg nyumbani kwa Abdilatif Abdalla.
Brother Moh vijana mfano wa mrangi na rodrick alexander wakikuona hapo kwenye picture wanastaajabu kwamba upande wako wa pili kumbe wewe ni mpiga piano? Hahaha wewe ni GOT kwenye Tasnia hii kongole kaka, unahistorisha, unafunza na kuburudisha
 
Makala...
GOT ni nini?

Utoto una mambo mengi.
Iikuwa ukiingia chumbani kwangu utakuta guitar Hoffner electrick.

Nikipigs guitar nikijaribu sana kukopi style ya Hank B. Marvin huyu alikuwa lead guitarist wa The Shadows hawa ndiyo wakmpigia Cliff Richard.

Utakuta viatu vya Addidas kwa ajili ya mpira.

Na blacbord ukutani kwa ajili ya masomo ya shule.

Ulikuwa wakati wake.
 
Makala...
GOT ni nini?

Utoto una mambo mengi.
Iikuwa ukiingia chumbani kwangu utakuta guitar Hoffner electrick.

Nikipigs guitar nikijaribu sana kukopi style ya Hank B. Marvin huyu alikuwa lead guitarist wa The Shadows hawa ndiyo wakmpigia Cliff Richard.

Utakuta viatu vya Addidas kwa ajili ya mpira.
Na blacbord ukutani kwa ajili ya masomo a shule.

Ulikuwa wakati wake.

WHAT DOES G.O.A.T. MEAN?​

Not many people can claim to be the G.O.A.T., but those who can are the Greatest Of All Time in their field. Most often, the acronym G.O.A.T. praises exceptional athletes but also musicians and other public figures.
On social media, it’s common to see the goat 🐐 emoji in punning relation to the acronym
 
Ahsante sana lakini sidhani kama nina sifa hiyo.
 
Pole sana ndugu lakini huyu mjomba wako hii haki miliki alisajiri...kama alisajiri huo ndio ushahidi wa haki yake vinginevyo ni ngumu kuamini!

Hilo la hati miliki ni jambo Moja, lakini kuhusu matibabu na stahiki zake Je?

Nirudie tu Kwa Mara nyingine kumpongeza Mzee wetu Mohamed Said Kwa uandishi murua na weledi lakini pia kuwa na subiria ya kufuatilia jambo bila kujiingiza kwenye kutetea kitu bila kupata taarifa zaidi. Mfano hapa ameomba apatiwe link ya Uzi asome taarifa kamili lakini pia amekiri Kuna kesi mahakamani akatahadharisha tusiongee mambo bila kuwa na ushahidi nayo.

Pole Kwa msiba wa Rafiki Yako Mzee wetu. Safari yetu sote.
 
Pole sana ndugu lakini huyu mjomba wako hii haki miliki alisajiri...kama alisajiri huo ndio ushahidi wa haki yake vinginevyo ni ngumu kuamini!
Brother Mohamed Said hawa jamaa wameleta tuhuma za "dhulma" kwa jamaa zako marhum "Shamte na kwikima", ila imenishangaza kuona mmoja analalamika kwamba mjomba wake alidhulumiwa haki miliki ya ugunduzi wa pombe huyu mwingine rodrick alexander yeye kaficha tuhuma zake, inasikitisha sana kaona kwenye Tanzia ya Shamte (Mola Amrahamu) ndipo pakubumbia tuhuma zake
 
Nikuambie tuhuma zake kama nani,, hata nikizitangaza keshatangulia mbele za haki hakuna kitakachobadilika.
Nimeshasema huyu mtu ana ndugu na familia yake si vizuri ukaanza kuongea hayo mambo wakati Kuna ndugu zake unachotafuta wewe ni umbeya tu wa kutaka kujua habari za marehemu.
 
If you wear a mask for too long, there will come a time when you can not remove it without removing your face.
Matshona Dhliwayo
 
Back
Top Bottom