Pole kwa Familia ya Mzee Mbuguni kwa Msiba huu na Mwenyezi Mungu aiweke Roho yake mahala pema peponi.
Nilimjua Marehemu na Familia yao mzima tokea nikiwa bado mdogo miaka ya 80 kuelekea ya 90 wakiwa Kwao Oysterbay nyuma ya Mtaa wa Chole ( Chole Road ) huku Marehemu akiwa ni Rafiki mkubwa wa Kaka zangu.
Pole nyingi sana pia kwa Dada yake ambaye anamiliki Benz Moja Kali sana ( labda kwa sasa awe ameshaiuza )kwani alishirikiana vyema nz Marehemu Kaka yake Kuiendesha hiyo Kampuni.
Luqman Maloto ni kweli kuwa Marehemu alifilisiwa ila ukisema kuwa Kafa Masikini nakukatalia kwani Marehemu anatoka Familia Bora ya Ushuani Oysterbay na Marehemu Baba yake aliwekeza katika Miradi mingi na Kuwasomesha vyema Watoto wake Wote huku baadhi yao wakiwa Kitengoni jirani na Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay.
Otherwise Hongera mno Luqman Maloto ( Mwanafunzi wangu katika Tasnia ) kwa Uandishi mzuri wenye Mpangilio wa Kitaaluma hasa ambao unamvutia Msomaji yoyote bila Kuchoka au Kumboa vile vile.
Katika Waandishi wa Habari wanaoujua Kuandika vyema, Kuchambua na kuweka Facts vizuri Luqman Maloto hukosi katika Tano Bora yangu na bahati nzuri GENTAMIYCINE nimekufundisha Tasnia hii Chuoni ( 2011 - 2012 ) hivyo nakujua Kiuwezo, Kitasnia na Kitabia na sishangai Wewe kuwa Bora na Mahiri hivi Kiuandishi.