Hii ni ya zamani sana lakini nimeona isiruhusiwe kuendelea kueneza uwongo bila kupingwa kwani unajenga hisia ya kuwa UDSM ilikuwa ni ya kipindi wewe uko pale tu chini ya Luhanga bila kuwa na picha kubwa cha chuo. Kulingana na record za
University of Dar es Salaam- mkuu wa kwanza wa chuo kikuu cha Dar es salaam tangu bado ikiwa ni College of East Africa alikuwa ni Ngwini (Dr Cranford Pratt) wa political Science. Huyu alifuatiwa na mganga wa biandamu (Dr WIlbert Chagula) ambaye aliondoka kwenye kiti hicho mwaka 1970 alipochaguliwa kuwa mbunge na kuteuliwa na Nyerere kuwa waziri wa Maji na Nguvu za Umeme (wakati huo). Kuanzaia mwaka 1970 hadi 1991 ambayo ni miaka 21 maVC wote wa wa UDSM ukianzia na Kaduma, Msekwa, Kuhanga na Mmari, wote walikuwa ni ngwini. Hata hivyo kipindi hicho ndicho ambachoo ndipo UDSM ilikuwa maarufu sana kwa Supps zikiitwa Cancun Conferences na madisco kibao. Vile vile ndipo wakati ambapo UDSM ilivutia wanazuoni maarafu sana sana kama akina Wadada Nabudere (Uganda), Mahamood Mamdani (Uganda), Walter Rodney (Guyana), Ali Mazrui (Kenya), Euphrace Kezirahabi (Tanzania) na wengine wengi.
Ingawa Luhanga alikaa madarakani muda mrefu sana, mchango wake (pamoja na Prof Mbwete ) ni kufanya transformation ya kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 3,800 hadi 18,000 na kuingiza siasa hizi za kuingilia maamuzi ya waalimu ili kupunguza percentages za disco. Wakati Luhanga anaanza madaraka tu mwaka 1991 niliwahi kuitwa na Prof Mrama ambaye ndiye alikuwa Chief Academic Officer wakati huo nijibu malalamiko ya mtoto mmoja aliyekuwa amedisco kwa kufeli masomo zaidi ya matatu, mojawapo likiwa la kwangu. Baada ya kumpa data, Mama Mrama akakubaliana na data nilizoweka mbele yake, yule mtoto akadisco ingawa alipata nafasi ya kujiunga na IDM Mzumbe wakati huo na kupasaua sana kwa diploma ya ADCA ya wakati huo.
Katika maisha yangu ya UDSM, nadhani viongozi nitakaowakumbuka sana ni Professor Mmari, Professor Msuya, Professor Mkude, Professor Mrama, na Professor G-Mgongo Fimbo.