Buriani Rosemary Kambarage Nyerere

Alafu wazee wengi wa zamani ndio zilikua itikadi zao. Hata kama tajiri, anakwambia mali ni zake, wewe ukuwe utafute vyako hana mpango na wewe. Ingekua mambo haya ya sasa nadhani mbaka kina edward nyerere wangekua mawaziri sahivi
 
Hii ni ya zamani sana lakini nimeona isiruhusiwe kuendelea kueneza uwongo bila kupingwa kwani unajenga hisia ya kuwa UDSM ilikuwa ni ya kipindi wewe uko pale tu chini ya Luhanga bila kuwa na picha kubwa cha chuo. Kulingana na record za University of Dar es Salaam- mkuu wa kwanza wa chuo kikuu cha Dar es salaam tangu bado ikiwa ni College of East Africa alikuwa ni Ngwini (Dr Cranford Pratt) wa political Science. Huyu alifuatiwa na mganga wa biandamu (Dr WIlbert Chagula) ambaye aliondoka kwenye kiti hicho mwaka 1970 alipochaguliwa kuwa mbunge na kuteuliwa na Nyerere kuwa waziri wa Maji na Nguvu za Umeme (wakati huo). Kuanzaia mwaka 1970 hadi 1991 ambayo ni miaka 21 maVC wote wa wa UDSM ukianzia na Kaduma, Msekwa, Kuhanga na Mmari, wote walikuwa ni ngwini. Hata hivyo kipindi hicho ndicho ambachoo ndipo UDSM ilikuwa maarufu sana kwa Supps zikiitwa Cancun Conferences na madisco kibao. Vile vile ndipo wakati ambapo UDSM ilivutia wanazuoni maarafu sana sana kama akina Wadada Nabudere (Uganda), Mahamood Mamdani (Uganda), Walter Rodney (Guyana), Ali Mazrui (Kenya), Euphrace Kezirahabi (Tanzania) na wengine wengi.

Ingawa Luhanga alikaa madarakani muda mrefu sana, mchango wake (pamoja na Prof Mbwete ) ni kufanya transformation ya kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 3,800 hadi 18,000 na kuingiza siasa hizi za kuingilia maamuzi ya waalimu ili kupunguza percentages za disco. Wakati Luhanga anaanza madaraka tu mwaka 1991 niliwahi kuitwa na Prof Mrama ambaye ndiye alikuwa Chief Academic Officer wakati huo nijibu malalamiko ya mtoto mmoja aliyekuwa amedisco kwa kufeli masomo zaidi ya matatu, mojawapo likiwa la kwangu. Baada ya kumpa data, Mama Mrama akakubaliana na data nilizoweka mbele yake, yule mtoto akadisco ingawa alipata nafasi ya kujiunga na IDM Mzumbe wakati huo na kupasaua sana kwa diploma ya ADCA ya wakati huo.

Katika maisha yangu ya UDSM, nadhani viongozi nitakaowakumbuka sana ni Professor Mmari, Professor Msuya, Professor Mkude, Professor Mrama, na Professor G-Mgongo Fimbo.
 
Unanikumbusha TAMBAZA mtoto wa mkuu wa Majeshi mwanae na wengineo walifanya Fujo walipigana na wanafunzi wa JITEGEMEE sijui AZANIA vile wakaumizan vibaya basi wakasimamishwa shule wakaambiwa wawaite wazazi wao waje nao
Huyo mtoto hakuna aliyejua kama ni mtoto wa mkuu wa MAJESHI
Ahmad MKUU WA MAJESHI huyo na walinzi wake Shule nzima macho pima MKUU WA MAJESHI kaitikia wito wa MZAZI
kufika kakaa anasubiri KIKAO CHA WAZAZI kianze mwalim mkuu hayupo anauliza kaenda wapi
Jibu kapewa kaitwa na WAZIRI WA ELIMU
akauliza kwa hiyo WAZIRI WA ELIMU ni muhimu kuliko wito alotuita sisi kiasi kashindwa kwenda muda mwingine
Mimi nimeitwa na RAISI(EDHI hizo Raisi mwinyi) na sijaenda nimeitikia wito wa MWALIMU kama mzazi
Inamaana huyu MWALIMU ametudharau sana sisi WAZAZI kwa kutupotezea muda
sasa akija umwambie yeye aje kwa kila mzazi nyumbani kwake kuongea nae ama lah kama hawezi jumatatu WATOTO wote warudi shule

Umenikumbusha mbali sana
 
Nimeshangaa umesema mcheshi wakati alipokuwa mbunge hakuwahi kuongea chochote hadi anamaliza ubunge.

Sikuwahi kujua alifika UDSM

Interesting
Aliwahi kutoa mchango wake bungeni juu ya viongozi wa Sengerema waliokuwa wanafyeka mahindi ya wakulima eti kuzuia mazalia ya mbu mjini... Alihoji sera ya kilimo nchini ni Kilimo Kwanza au Mbu Kwanza. Bunge Iote waliangua vicheko na makofi. Shida yetu hautufuatilii Bunge.
 
Mbona hujaweka chanzo cha habari yako. Au unataka kutuaminisha ww ndio uliupiga nae? Kwa uandishi huu mhh napata ukakasi
 
Nimeshangaa umesema mcheshi wakati alipokuwa mbunge hakuwahi kuongea chochote hadi anamaliza ubunge.

Sikuwahi kujua alifika UDSM

Interesting
Aliwa hi na ali kuwa na kinzana sana na Waziri Rita Mlaki kwnye maswali na majibu. Nina kumbuka wakati bado nina ujiko wa cheo cha babangu , nilikutana naye hapo JKN airport VIP, mimi nilikuwa na mama yangu tuna safiri kwenda UK na yeye alikuwa ana kwenda Cuba , tulisafiri ndege moja tukaachana Amsterdarm ninadhani alikuwa na mume huko CUba na kipindi hich alikua mkono wake bado ume fungwa hogo baada ya kuvamiwa na majambazi na kumjeruhi mkono .
 
Sema ukweli kuwa alikuwa shemeji yetu bwana we mbona umezunguka sana. Pole ndugu yetu Kwa kufiwa na shemeji yetu
 
Siku hizi Walimu kazi ya awali baada ya kupokea Mwanafunzi mpya ni kuuliza kazi ya Wazazi ili ageuke chawa wa Mwanafunzi
 
Heshima sana kwako mkuu Kichuguu.
 
Hapana she was far from Newton

Muhimu kujua hawakutelekezwa

Alipewa ubunge .. angekuwa active angepewa zaidi vyeo vingine.

But alikuwa so silent
Wanaojua wanasema alipopata Ubunge alikua na sonona la moyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…