BURIANI Sultan Jamshid BIN Abdulla BIN Khalifa (1926 - 2024)

Huyu Mzee kila siku anamdisi Mwalimu Nyerere aliyeongoza harakati za uhuru wetu, ila huyu hapa anamsifia Sultani aliyepinduliwa kwa kuwanyima haki za kisiasa n.k wazanzibar.
Kisa na mkasa; Dini.
Mkuu suala kuu la mwandishi huyu wa hii taazia ni DINI.

As far ni ndugu yake ktk imani hata kama ni magaidi ya Houthi, hezbollah, alshabab, al qaeda n.k atawapamba
 
Story za kwenye vijiwe vya kahawa hizo
 
Chivundu,
Imetokea kuwa nimetafiti vya kutosha historia ya mapinduzi nikiwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany kuanzi 2003 hadi 2010.

Nimekuwepo katika mahojiano yake na wahusika wakuu wa mapinduzi Tanga na Dar-es-Salaam.

Mimi ndiye niliyemfikisha Daktari Kipumbwi kulipokuwa na kambi ya Wamakonde waliovushwa kuingia Zanzibar kusaidia mapigano mwaka wa 1964.

Historia yote ipo katika kitabu alichoandika Dr. Ghassany, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."

Ikiwa utakuwa mstaarabu na kujiepusha na lugha za kejeli za "kufurushwa," tunaweza tukafanya mjadala wa kiungwana utakaowanufaisha wengi hapa jamvini.

Nina ujuzi wa kutosha kiasi nimealikwa Zanzibar mara tatu kufanya pitio za vitabu vya mapinduzi hadharani na nikajaza ukumbi pomoni.

Mbali na makala na mahojiano ninayofanya kwenye televisheni na radio za ndani na nje kuhusu historia ya Zanzibar.

Masultani hawakupata kuua Wazanzibari wala kuweka jela za mateso Zanzibar.

Hawana historia hii katika utawala wao wote.
 
Sawa mwema alikuwa baba yako Nyerere aliyeuwa watu kwa maelfu pamoja na kuweka legacy ya mauwaji yanayofanywa na CCM mpaka leo
 
Mkuu suala kuu la mwandishi huyu wa hii taazia ni DINI.

As far ni ndugu yake ktk imani hata kama ni magaidi ya Houthi, hezbollah, alshabab, al qaeda n.k atawapamba

Kwani unafikiri lengo la mavamizi ya Zanzibar nalo lilikuwa nini si hiyohiyo dini
 
Unauliza wakati unaambiwa keshakufa? Au unataka habari za ziara ziendelee ili iweje?
ili tumuone huyo sultan, kining'ina wa sultan seyyid said toka oman aliyehamia zanzibar na kuanza kuitawala
 
Kwani unafikiri lengo la mavamizi ya Zanzibar nalo lilikuwa nini si hiyohiyo dini
Lengo lilikuwa nikumrushia sultan na uarabu wake kwao .
Wabaki waafrica weusi halisi
 
Hichi kitu cha Sultan na wazanzibar kuwinda nguruwe wa kitoweo kimenishtua sana.
Kumbe Sultani na wazanzibar kiasili walikuwa ni walaji wazuri mnoo wa kitimoto.
Mzee saidi mbona hizi siri hukutupa tangu kitambo?

Wazanzibar sasa tuache unafiki, kitimoto ipatikane wazi na popote Zanzibar. Ni urithi wetu huo.
 
Alikuwa mtu mwema sana.Mzanzibar halisi,muongea kiswahili fasaha.Hakika propaganda zilizopigwa na ccm zilitunyima mambo mengi mazuri.Mungu amazed pema peponi.
 
Sultan alinyang'anya haki za watu Kwa kuwa kwao ni Oman kwanini aje atawale ardhi ya watu wengine?
Sultan aliyetoka Oman siyo Jamshid,Jamshid ni kizazi cha mbali sana cha babu wa mababu zake yeye.Sultan wa Oman na Zanzibar ni Seyyid Said aliyefariki 1856.Hapo ufalme wake uligawanywa pande mbili ,Zanzibar alirithi Sultan Majid na Sultan Thuwein ,Oman. JAMSHID alikuwa mswahili na Mtanzania kama sito Fiona na ghilba za CCM.Jamshid alikuwa Sultan kwa mujibu wa katiba,hakuwa mtendaji wa serikali,serikali ilikuwa chini ya waziri mkuu,Mohamed Shamte ambaye mwanaye Adam Shamte amekuwa kada wa kudumu wa CCM.Harakati za uhuru wa Zanzibar zilihusisha ubaguzi wa rangi hivyo chama ZNP kilikuwa karibu zaidi na sultan lakini hata ASP kisingeweza kusajiriwa bila kumtambua sultan kama head of state.Yaliyotokea 1964 ni ghiliba za majirani hasa Tanganyika na waingereza.Zanzibar haikutakiwa tena kuwa sovereign.
 
Lengo lilikuwa nikumrushia sultan na uarabu wake kwao .
Wabaki waafrica weusi halisi
Kwani mwarabu alikuwa na serikali toka lini? Tafuta kitabu cha Padri Sivallon kinaitwa Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania bara , utajuwa nini lengo la kanisa
 
Kwani mwarabu alikuwa na serikali toka lini? Tafuta kitabu cha Padri Sivallon kinaitwa Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania bara , utajuwa nini lengo la kanisa
Lengo la kanisa ktk nini?! Usultani au utawala wa zanzibar kama mada isemavyo?!
 
Duu! Kwahiyo upo radhi ungetawaliwa na Sultan kutoka Oman kuliko kujitawala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…