BURIANI Sultan Jamshid BIN Abdulla BIN Khalifa (1926 - 2024)

BURIANI Sultan Jamshid BIN Abdulla BIN Khalifa (1926 - 2024)

View attachment 3189131
(1929 - 2024)​

Hiyo taazia hapo chini niliandika majuma machache yaliyopita nilipopokea taarifa kuwa Sultan Jamshid kafariki.

Haukupita muda nikapokea taarifa kuwa si kweli yu hai.
Nilijisikia vibaya sana.

Ninachokumbuka ni kupokea ujumbe kutoka kwa rafiki yangu akiniambia nilifanya haraka kuandika.

Sikuwa na la kusema.
Nilibakia kimya.

Niliandika taazia wakati Sultan Jamshid yu hai.
Taazia niliyoiandika ni hiyo hapo chini:

Jana usiku ndugu yangu kaniletea ujumbe mfupi kuwa Sultan Seyyid Jamshid, Sultani wa mwisho wa Zanzibar kafariki.

Asubuhi ndugu yangu huyu akanipigia simu tukazungumza mawili matatu akanifahamisha kuwa yeye hakupata kuonana na Jamshid ila alizungumzanae mara moja kwa simu Jamshid alipokuwa anaishi Portsmouth.

Sasa nikawa najiuliza nini naweza kuandika kuhusu Sultan Jamshid.

Jamshid kaandikwa sana kiasi nimekumbuka maneno ya marehemu Bibi Titi Mohamed aliponiambia, "Bwana Mohamed kipi utakachoandika wewe kuhusu mimi ambacho bado hakijaandikwa?"

Kipi ninachoweza mimi hii leo kuandika kuhusu Sultan Jamshid ambacho bado hakijaandikwa?

Kipo cha kuandika kuhusu Sultan Jamshid bin Abdulla bin Khalifa ambacho bado hakijaandikwa.

Jamshid kaondoka Zanzibar baada ya mapinduzi nafsi yake ikiwa imesalimika.
Jamshid anakwenda kwa Mola wake vidole vyake vikiwa safi havichuruziki damu.

Hakuna Mzanzibari anaeweza kusimama akasema Sultani ameniulia ndugu yangu au Sultani kanidhulumu haki yangu hii au ile.

Jamshid kaondoka Zanzibar hakuacha jela za mateso.
Jamshid hakuacha jela za mateso kwa kuwa hakurithi jela ya mateso.

Jamshid hakupata kukalia kiti cha enzi kilicholowa damu.
Hakika lipo la kuandika na la kusema kuhusu Jamshid.

Nimeingia Maktaba.
Natalii farahasha ya kitabu cha Harith Ghassany, "Kwaheri Uhuru Kwaheri Ukoloni."

Nataka nijikumbushe.

Najikumbusha kwa kuwa nilikuwa msaidizi wa Dr. Ghassany wakati wa utafiti wa kitabu hiki chake.

Nasoma yaliyomfika Jamshid halikadhalika nayasoma yale waliyopitia Wazanzibari waliokuwa nje ya Zanzibar mapinduzi yalipotokea.

Nayasoma na kuona kama vile ndiyo kwanza hayo nisomayo nayasikia leo.
Sultan Jamshid kapewa hifadhi Dar es Salaam yeye na familia yake na baadhi ya watu.

Wako wamejibanza kwenye nyumba mbili jumla yao watu 43.
Serikali ya Tanganyika inafanya mawasiliano na Waingereza kuhusu Sultan Jamshid.

Jamshid Sultan wa Zanzibar ni mtu masikini kwani hana fedha nje ya Zanzibar hata senti moja.

Sultan hana nauli ya kumfikisha Uingereza.

Nimetosheka.
Navuta kitabu kingine ninachokumbuka kuna habari za Sultan Jamshid.

Hili ni buku la mapicha kutoka matoleo ya gazeti maarufu DRUM lililokuwa likimilikiwa na Jim Bailey kutoka Johannesburg, Afrika Kusini.

Nilisaidia kuhariri na kuchapwa kwa kitabu hiki.

Katika kitabu hiki kuna makala ya Jamshid akiwa na watu wapatao 500 wananchi wa kawaida wanaingia porini kuwinda nguruwe.

Sultan Jamshid anaingia porini kwenye msitu mzito bila ulinzi wowote kuwinda pamoja na wawindaji wenzake wamemzunguka wamebeba mikuki.

Hakika yako mengi ya kusema kuhusu Jamshid.

Sura inayofuatia katika DRUM ni kuhusu mapinduzi chenye kichwa cha habari, "Bloodshed on the Spice Isle."

Nahitimisha safari yangu Maktaba kwa kitabu muhimu sana katika historia ya masultani: "Omani Sultans in Zanzibar," kilichoandikwa na Ahmed Hamoud Al Maamiry.

Mwanzo wa kitabu mwandishi anasikitika kuhusu damu iliyomwagika katika mapinduzi.
Siku zote historia ya mapinduzi itakuacha na majonzi.

Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi hisabu yake ndugu yetu Sultan Jamshid bin Abdulla bin Khalifa.

View attachment 3189147

Najalibu kuwaza,what is so special about this Arab/Muslim reader? Yani mgeni aliyekuja aka watawala, mkawa vijakazi wake, Leo hii mnaonesha mahaba kwake! Kwamba mnaona ni Bora aje awatawale tena!!?
Kuna miundombinu Ali Jenga? Elimu, afya,uchumi, nk, au ndio Stockholm Syndrome, you fall in love with ur oppressors, kuna wa Swahili weusi waliperekwa utumwani Arabia, wakaishia kuminywa makende ili wasizaliane! Ili haliwapi tsbu kisa tu, ya uislam/uarab?
Mkrsito yoyote,anaona myahudi kama super race, taifa la Mungu, hata liuwe vipi watoto na wana wake wa Gaza, kwa mkrsito ni sawa tu, wayahudi hawa hawa, kipindi cha apartheid SA, waliwatumia watu weusi kwenye majaribio ya dawa za sumu!
Watu weusi mna shida gani vichwani?
Kwanini dini zinawafanya mnakuwa mazombi,?
 
Vile ukute hata waingereza waliotutawala walikuwa watu poa tuu,
 
Utawala uliopinduliwa si wa Sultani kama CCM na Nyerere wanavyowadanganya, Iliyopinduliwa ni serikali ya Waziri mkuu Muhammed Shamte , Mpemba wa Ole. Alikamatwa na Nyerere na kufungwa zaidi ya miaka 10 jela huko Tanganyika bila ya kufikishwa mahakamani, waliofungwa ni pamoja na baraza lake la mawaziri .

Yaani Watanganyika mna damu mikononi mwenu na deni kubwa sana kwetu Wazanzibari
Hapo cjaelewa kuhusu Mohamed shamte na Huyo Sultan
 
Najalibu kuwaza,what is so special about this Arab/Muslim reader? Yani mgeni aliyekuja aka watawala, mkawa vijakazi wake, Leo hii mnaonesha mahaba kwake! Kwamba mnaona ni Bora aje awatawale tena!!?
Kuna miundombinu Ali Jenga? Elimu, afya,uchumi, nk, au ndio Stockholm Syndrome, you fall in love with ur oppressors, kuna wa Swahili weusi waliperekwa utumwani Arabia, wakaishia kuminywa makende ili wasizaliane! Ili haliwapi tsbu kisa tu, ya uislam/uarab?
Mkrsito yoyote,anaona myahudi kama super race, taifa la Mungu, hata liuwe vipi watoto na wana wake wa Gaza, kwa mkrsito ni sawa tu, wayahudi hawa hawa, kipindi cha apartheid SA, waliwatumia watu weusi kwenye majaribio ya dawa za sumu!
Watu weusi mna shida gani vichwani?
Kwanini dini zinawafanya mnakuwa mazombi,?
Juan...
Stockholm Syndrome na utawala wa Sultani Zanzibar havioani.

Wala Sultani hakuwatesa raia wake.

Isome historia ya Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi.
 
Hapo cjaelewa kuhusu Mohamed shamte na Huyo Sultan

Serikali iliyopinduliwa si ya Sultani , ni serikali iliyochaguliwa kihalali chini ya Tume huru ya uchaguzi , na wala haikupinduliwa ilivamiwa na Nyerere. Ni kama leo hii useme serikali ya King charles imepinduliwa uingereza wakati serikali ya uingereza haiongozwi na King Charles , inaongozwa na Stammer na ni ya chama cha Labour.
 
Serikali iliyopinduliwa si ya Sultani , ni serikali iliyochaguliwa kihalali chini ya Tume huru ya uchaguzi , na wala haikupinduliwa ilivamiwa na Nyerere. Ni kama leo hii useme srikali ya King chrles imepinduliwa uingeteza wakati serikali ya uingereza haiongozwi na King Charles , inaongozwa na Stammer na ni ya chama cha Labour.
Hujajibu swali vizuri, nimeuliza kuhusu Sultan na Na huyo waziri mkuu , mapinduzi yalifanyka kwa Sultan au Waziri mkuu?
 
Much...
Mipango ya mapinduzi ilifanyika Tanganyika na Zanzibar.

Tanganyika sehemu inayoitwa Kipumbwi, Tanga iliwekwa kambi ya Wamakonde kutoka Shamba la Mkonge la Sakura kuwafunza mbinu za kupigana.

Hawa Wamakonde walivushwa kuingia Zanzibar kushiriki uchaguzi na mwaka wa 1964 walishiriki kama askari mamluki kupindua serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.
Kwan wamakonde nao si waislam? Hata hao wazee ambao mliwahoji kwenye icho kitabu wote ni waislamu... Naona unajaribu sana kuficha ukwel uo kwa kusema eti wamakonde, Sema wamakonde waislamu... Ingawa hii nayo si kwel

Ukisikiliza mahojiano na Shekhee Mahsin atasikia anasema kwa mdomo wake siku ya Mapinduzi watu walivamia ghala la silaha wakiwa na mikuki.... yaan Tanganyika tupange Mapinduzi kisha tuwape watu mikuki??? Punguza chuki na udini wee mzee.
 
Proved,
Uongozi wa ASP ulishirikiana serikali ya Tanganyika kufanikisha Mapinduzi.

Halikadhalika Makomredi yaani Umma Party walitoa michango wao kuonyesha njia pale walipoingia kati kukomesha mauaji.
Proved? How...!
Kwamba Nyerere aliwapa watu mikuki na mishale wakapindue?
 
Hujajibu swali vizuri, nimeuliza kuhusu Sultan na Na huyo waziri mkuu , mapinduzi yalifanyka kwa Sultan au Waziri mkuu?
Aliyepinduliwa ni waziri Mkuu kwani alikamatwa yeye na mawaziri wake na kufungwa Tanganyika kwa Nyerere kwa miaka zaidi ya kumi.

Sultani alipokelewa na Nyerere kwa zulia jekundu na Muingereza kuleta ndege ya kumchukuwa mpaka Uingereza.

Baadhi ya Waliofungwa baada nchi kuvamiwa na Nyerere ni hawa. Walifungwa bila kufikishwa mahakamani


MAHABUSU WA KISIASA WA MWALIMU NYERERE

Maalim Harun Ustadh
Maalim Mohammed Mattar
Seyyid Hassan Sheikh
Seyyid Mohammed Adnan
Mzee Mohammed Mbaba
Ahmed-Rashad Ali
Hashim Haji Abdalla
Seyyid Hashim Abdalla Baharun
Abdul-Latif Binbrek
Mohammed Shioni
Seyyid Mohammed Mattar
Mohammed Ali Abbas
Ali Abdalla (Admeri)
Ali Jaffer
Ali Khalifa Miskiry
Ali Manara (Mtu wa Tanganyika)
Aman Thani Fairooz
 
Back
Top Bottom