Burkina Faso: Jeshi lampindua Rais Kabore. Lasimamisha Katiba na kuvunja Serikali

Burkina Faso: Jeshi lampindua Rais Kabore. Lasimamisha Katiba na kuvunja Serikali

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1643094698367.png


1643094754515.png


Mbali na kusema Rais Roch Kabore amepinduliwa Jeshi Nchini humo pia limesema Bunge limevunjwa na Mipaka ya Taifa hilo imefungwa.

Uamuzi huo umesainiwa na Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba. Jeshi limesisitiza Mapinduzi yamefanyika bila ghasia na watu wanaoshikiliwa wapo sehemu salama.

Kauli ya Jeshi inakuja baada ya siku mbili za sintofahamu na hofu katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Ouagadougou ambapo risasi zimekuwa zikisikika.

=====

Burkina Faso's army said on Monday it had ousted President Roch Kabore, suspended the constitution, dissolved the government and the national assembly, and closed the borders.

The announcement, signed by Lieutenant Colonel Paul-Henri Sandaogo Damiba and read by another officer on state television, said the takeover had been carried out without violence and that those detained were at a secure location

The statement was made in the name of a previously unheard of entity, the Patriotic Movement for Safeguard and Restoration or MPSR, its French language acronym.

"MPSR, which includes all sections of the army, has decided to end President Kabore's post today," it said.

It cited the deterioration of the security situation and what it described as Kabore's inability to unite the nation and effectively respond to the challenges it faces.

The army broadcast came after two days of confusion and fear in the capital Ouagadougou, where heavy gunfire erupted at army camps on Sunday, with soldiers demanding more support for their fight against Islamist militants.

Kabore's whereabouts were unknown on Monday after heavy gunfire was heard in the area around his residence overnight.

Earlier, Kabore's party said he had survived an assassination attempt, but gave no details.

Before the army statement, the African Union and the West African bloc ECOWAS both condemned what they called an attempted coup in Burkina Faso, saying they held the military responsible for Kabore's safety.

Source: Reuters
 
Hilo jeshi linapenda raia wao, kwanini wakimbatie dictator wakati wananchi wanateseka, hao viongozi kama wakina Museveni lazima wapinduliwe
 
Amechelewa sana kupinduliwa; why wait for so long? Do the right thing at the right time! Mnajivuta mno nyie jeshi! Msisahau kwamba mpo kwa ajili ya kuwalinda raia na mali zao. Watawala wakiwa walafi na wabinafsi, wafurumusheni haraka kunako alfajiri na mapema!
 
Africa kumekucha !

Ipo haja watawala kujiangalia Mara kadhaa utendaji wa majukumu Yao.
Siyo kujiangalia. Hao wanajua KIMBIA FIKA wanachofanya! Watawala wanapaswa kutimiza matakwa ya wananchi waliowaweka madarakani, na wala si kutumikia matumbo yao yasiyotosheka shibe!
 
Miafrika ndio tulivyo.
Mambo ya kishenzi kila kukicha,na kote mapinduzi yalikofanyika hakuna cha maana wala unafuu wa maisha umeletwa.

Hapo ni majeshi kutafuta tuu vyeo vya kisiasa na kutafutia familia zao Kazi ila wananchi wajinga wataishia kushangilia na kuambulia hewa.

Binafsi ni mmja wa watu naopinga kabisa majeshi kwenye siasa maana hata wakiharibu hakuna cha Kuwafanya wameshika silaha.

Hii tabia imekithiri Sana kwenye Nchi za francophone.
 
Siyo kujiangalia. Hao wanajua KIMBIA FIKA wanachofanya! Watawala wanapaswa kutimizwa matakwa na wananchi waliowaweka madarakani, na wala si kutumikia matumbo yao yasiyoshiba!
Matakwa wanajitajidi kutimiza ila huwezi furahisha kila mtu au kila kikundi..

Sasa majeshi ndio yatatimiza? Si inakuwa ni sawa na kusema tukose wote au wote tule msoto..

Mwisho wa.siku.mlichokuwa mnaona kibaya kwa raia ndio itakuwa mbaya zaidi kwa wanajeshi na hakuna wa kuwatetea na wao hawachunguzwi wala hakuna wa kiwanyoshea mkono wanafanya watakacho.
 
Matakwa wanajitajidi kutimiza ila huwezi furahisha kila mtu au kila kikundi..

Sasa majeshi ndio yatatimiza? Si inakuwa ni sawa na kusema tukose wote au wote tule msoto..

Mwisho wa.siku.mlichokuwa mnaona kibaya kwa raia ndio itakuwa mbaya zaidi kwa wanajeshi na hakuna wa kuwatetea na wao hawachunguzwi wala hakuna wa kiwanyoshea mkono wanafanya watakacho.

Ushauri pekee n'aoweza kukupatia ni kwamba: FUMBUA MACHO YAKO! You seem to have been slumbering for too long!
 
Mbali na kusema Rais Roch Kabore amepinduliwa Jeshi Nchini humo pia limesema Bunge limevunjwa na Mipaka ya Taifa hilo imefungwa

Uamuzi huo umesainiwa na Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba. Jeshi limesisitiza Mapinduzi yamefanyika bila ghasia na watu wanaoshikiliwa wapo sehemu salama...
Safi kama Rais ni kibaraka yupo kwa maslahi ya kikundi au taifa fulani anamng'olewa kwa maslahi ya taifa
 
Jeshi nchini Burkina Fasso linasema kwamba limechukua mamlaka na kumuondoa madarakani rais Roch Kabore.

Tangazo hilo lilitolewa katika runinga ya taifa na afisa mmoja wa jeshi , ambaye alisema kwamba aserikali na bunge limevunjwa.

Kufikia sasa haijulikani bwana Kabore yuko wapi , lakini afisa huyo amesema kwamba wale wote wanaozuiliwa wapo katika eneo salama.

Mapinduzi hayo yanajiri siku moja tu baada ya wanajeshi hao kudhibiti kambi za jeshi huku milio ya risasi ikisika katika mji mkuu wa Ouagadougou..

Mapema , Chama tawala cha peoples Movement PMP kilisema kwamba wote Kabore na waziri mmoja wa serikali walinusurika jaribio la mauaji.

Siku ya Jumapili, wanajeshi waasi walitaka kufutwa kazi kwa maafisa wa jeshi na kuongezwa kwa raslimali za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu.

Taarifa hiyo ilitolewa na kundi ambalo halijasikika hapo awali, Vuguvugu la Patriotic for Safeguard and Restoration au MPSR, kifupi chake cha Kifaransa.

"MPSR, ambayo inajumuisha vitengo vyote vya jeshi, imeamua kusitisha wadhifa wa Rais Kabore leo," ilisema.

Kabla ya tangazo hilo, Muungano wa Afrika na Umoja wa Afrika Magharibi Ecowas walilaani kile walichokiita jaribio la mapinduzi nchini Burkina Faso.

Ecowas imesema kwamba wanajeshi watawajibikia usalama usalama wa Bw Kaboré iwapo lolote litatokea.
Video kutoka mji mkuu inaonekana kuonyesha magari ya kivita - yanayoripotiwa kutumiwa na rais - yakiwa na mashimo ya risasi na kutelekezwa mitaani.

Huduma za mtandao wa simu za mkononi zimekatizwa, ingawa mtandao wa laini zisizobadilika na wi-fi ya nyumbani zinafanya kazi

Bw Kaboré hajaonekana hadharani tangu mzozo huo uanze lakini machapisho mawili yalionekana kwenye akaunti yake ya Twitter kabla ya afisa huyo kutangaza kuwa amepinduliwa.

Baadaye alitoa wito kwa wale waliochukua silaha kuziweka chini "kwa maslahi ya taifa". Hapo awali Bw Kaboré alipongeza timu ya taifa ya kandanda kwa ushindi wao katika mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Haijulikani ikiwa Bw Kaboré au mtu mwingine alichapisha tweets hizo.

Baadhi ya vyanzo vya usalama vinasema rais na mawaziri wengine wa serikali wanazuiliwa katika kambi ya Sangoulé Lamizana katika mji mkuu.

Siku ya Jumapili, mamia ya watu walijitokeza kuwaunga mkono wanajeshi hao na baadhi yao walichoma moto makao makuu ya chama tawala. Amri ya kutotoka nje wakati wa usiku imewekwa.
 
Back
Top Bottom