Burna Boy ni zaidi ya Wizkid na Davido kwa sasa?

Kwahyo amewazidi Kidayo na Obo kwa sasa huku Afrika?

Brother kwa era hii Burna ni habari nyingine asee hivi unajua wiki kama mbili zilizopita kaweka rekodi yake ya kujaza Arena huko Uingereza?

Mafanikio ya msanii sio kwenye views, followers na skendo, fuatilia historia ya Burnaboy jamaa alikuepo kitambo tu sema hakuwai wika kiivyo nliwai soma documentary flan wanasema jamaa alianza imba ana 10 yrz na 19 yrz alikuwa anaendesha Range.

Huyu jamaa ana management ya kipekee kwanza mama yake ndio msimamizi wa kazi zake na show kwa ujumla, wanakwambia hata matumizi ya simu kwa jamaa wanacontrol na Management na simu yake wamemuachia Whatsapp tu. Angalia katika account ya Jamaa vitu anavyopost kama sio show na picha za akiwa anatumbuiza au yuko katika harakati za kwenda tumbuiza, kwangu Mimi Burna ni Mkali sana kuliko hata hao kina Davido wanaotumia nguvu nyingi kupambana just imagine jamaa kaja na style yake na kapenya simple tu
 
Ni wakati wa Burna Boy kung'ara baada ya msoto sana mwaka 2016 alitaka kuacha mziki kabisa
 
Kila mtu anawakati wake wa kutamba
Utakuwa umemjua Burna boy Leo wewe... Jamaa huko UK kaanza kitambo zaidi ya Huyo Wizkid ... Kaisikilize Album yake ya African Giant Ni Moto. Kwa taarifa yako Jamaa mwaka 2019 kaumaliza hivi. Nakukumbusha tu jamaa Hana mambo ya Kick kupush mziki wake licha ya kuwa anatoka na demu mkali Steflon Den. Acha niendelee kusikiliza Goma lake Jipya Yuko na Eddy Sheran amelidondosha Jion Hii.

 
Gud ngoja tumsubiri kwenye International Collabo.
 
Ngoma ni ya Stomiz ft Ed Sheeran&Burna Boy
 
Acha kulinganisha hizo takataka na Egbe Egbe Burna Boy .... Yaani unamlinganisha Korede Bello Na Burna .. Wewe Jamaa acha mambo yako humjui Burna Wewe...
 
Hawajawahi kushuhudia Show za jamaa ..



Na Burna haimbi Mainstream Music atabaki juu Sana , toauti na hawa wengine wanaimba muziki unaoendana na muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…