Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amekataa hoja ya Katiba Mpya inayosisitizwa na baadhi ya vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, akisema wananchi hawahitaji Katiba Mpya.
Aidha, Faris amekosoa baadhi ya kauli zinazotolewa na CHADEMA katika ziara zake, akidai kuwa chama hicho kimekuwa kikieneza chuki na kumtukana Rais kwa madai kwamba ana mamlaka makubwa, jambo ambalo amesema si kweli.
Buruan amefafanua kuwa wananchi wanahitaji huduma muhimu kama vile maji safi, barabara bora, na huduma bora za afya badala ya kujaza vichwa vyao na mijadala ya katiba. Amedai kuwa wanaopigia kelele katiba mpya wanalenga mambo mawili tu binafsi:
1. Kubadilisha Tume ya Uchaguzi ili wapate madaraka na
2. Kupunguza madaraka ya Rais.