Burundi: Kampeni za uchaguzi zaanza rasmi nchini

Burundi: Kampeni za uchaguzi zaanza rasmi nchini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kampeni za uchaguzi wa urais utakaofanyika Mei 20 zimeanza leo, Aprili 28 nchini Burundi. Mgombea urais kupitia chama tawala CNND-FDD, Evariste Ndayishimiyena na Agathon Rwasa wa chama cha upinzani, CNL wamezindua kampeni zao

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi (CEN), Pierre Claver Kazihise, amewaonya vikali wale wote watakaokwenda kinyume na sheria, huku waziri wa afya akiwakumbusha wagombea na raia kuzingatia kanuni za kuepukana na ugonjwa wa #COVID19

Mgombea wa chama tawala tayari amepata uungaji mkono kutoka vyama vya FNL kinachoongozwa na Jaques Bigirimana, muungano wa COPA, na wafuasi wa UPRONA wanaounga mkono kundi la Isidore Mbayahaga

Waziri wa Usalama Alain Guillaume Bunyone amewataka wagombea kujiepusha na kauli za uchokozi zinazoweza kuhatarisha usalama

Kampeni hii iloanza leo itamalizika Mei 17 . Wagombea 7 kiti cha urais wameorodheshwa na CENI, mgombea wa chama tawala, Evariste Ndayishimiye, na wa chama cha upinzani cha CNL, Agathon Rwasa, wakitabiriwa kuchuwana vikali
1588081502220.png

1588081515050.png


1588081531202.png
 
Virusi vya corona: Mikutano mikubwa ya Kampeni za uchaguzi zaibua hofu ya maambukizi ya virusi vya corona

Jumatatu katika mji wa Gitega watu walikua wemejaa kiasi cha kubaba wakati wa kampeni za mgombea wa chama tawala

Jumatatu katika mji wa Gitega watu walikua wemejaa kiasi cha kubaba wakati wa kampeni za mgombea wa chama tawala
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES Image

Picha zinazoonyesha mikusanyiko ya maelfu ya watu waliokusanyika Jumatatu kwa uzinduzi wa mikutano ya kampeni za kisiasa nchini zimeibua wasi wasi mkubwa ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona kabla ya taifa hilo kufanya uchaguzi unaotarajiwa tarehe 20 Mei mwaka huu.

Mikutano mikubwa ilishuhudiwa jana katika mji wa kisiasa wa Gitega ambako chama tawala cha CNDD-FDDB, pamoaja na mkoa wa Ngozi uliopo Kaskazini mwa nchi ambako wapinzani wakuu walizindua kampeni zao.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humoimetoa sabuni na ndoo kwa wagombea wa uchaguzi ilivitumiwe na wafuasi wao kunawa mikono wakati wa kampeni , wakati mmoja pia kemikali za kuua vimelea pia zilitumika.

Lakini "idadi ya watu waliohudhuria mikutano hiyo ilikuwa kubwa mno kiasi cha kutotoshwa na maji na vitakasamikono vilivyokuwepo " mmoja waliohudhuria mkutano wa kampeni katika mkoa wa Kirundo ameiambia BBC.

Katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu walielezea hofu zao huku wakiishutumu serikali kwa kuhatarisha maisha ya watu:

'Hakuna tisho la kutosha kuahirisha uchaguzi'
Serikali ya Burundi imefunga mipaka yake ili kuzuwia kusambaa kwa virusi, na kurugusu shehena za malori ya mizigo tu kuingizwa nchini kutoka mataifa jirani.

Ndaniya nchi, watu wameshauriwa kutosalimiana kwa mikono na kunawa mikono mara kwa mara, na maisha yanaendelea kama kawaida.

Taifa hilo limerekodi visa 14 vya Covid-19, na serikali imesisitiza kuwa bado hakuna tisho la kuifanya iahirishe uchaguzi mkuu.

Alipotazama picha za mikutano ya kisiasa, Dkt Olivier Manzi mtaalamu wa mamgonjwa ya maambukiziameiambia BBC kuwa hayo ni maeneo yanayoweza kuwa kitovu cha maambukizi ya virusi vya corona.

Image caption Baadhi ya watu waliokua wamehudhuria kampeni za mgombea wa chamacha upinzani cha CNL katika mkoa wa Ngozi
Dkt. Manzi ambaye anafanya kazi katika Shirika la Afya Duniani (WHO), ameiambia BBC kuwa mikusanyiko hiyo ni maeneo yanayosambaza kwa kasi virusi vya corona.

"Kwa mfano nchini Senegal, kulikua na visa vichache mwanzoni lakini baada ya mikusanyiko mikubwa ambayo ilitokea idadi ya visa ilipanda haraka, hii pia imeshuhudiwa katika baadhi ya mataifa mengine " - anasema Daktari Manzi.

Nchini Italia, mechi ya soka katika uwanja wenye uwezo wa kuchukua watu 44,000 wa San Siro tarehe 19 Februari kati ya Atalanta Bergamo na Valencia kutoka Uhispania inaamiwa kuwa chanzo cha kuenea kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya corona kaskazini mwa nchi hiyo.

"Hilo ni bomu lisiloonekana. Hatukujua virusi vinazunguka miongoni mwetu" - Giorgio Gori, meya wa Bergamo aliliambia jarida la michezo la Marca.

Chanzo: BBC Swahili
 
Kumbe tuna ahueni!!
😂😂
Nchi nyengine bhana utafikiri wanaishi mbinguni kumbe hapo tu karibu na tz! Hawa ndo wanafaa kuambiwa tusitishane.
 
Burundi hawaeleweki hawa jamaa. Ukiangalia mipakani mwao yaani ulinzi uko very strictly.. yaani askari wa kirundi hataki hata kumsogelea mTZ unakaa mita kama 2 ndio mnaongea.

Juzi nilikua mpakani yaani jamaa wanonekana wamejipanga kweli kweli. Sasa leo ninapoona post hio nashindwa kuwaelewa kabisa wanamaanisha nini kukomaa vile mipakani halafu wanalegeza ndani.
 
Corona inathibitiwa mipakani! Tanzania tulifanya uzembe kuthibiti mipaka.

Burundi walithibiti mipaka kweli kweli kuna kipindi walikuwa wanawarudisha warundi mipakani walipotoka. Hawana Mzaha mipakani kama sisi na kenya tulivyofanya so inawezekana wagonjwa wapo sehemu moja under control.

Pia Mkumbuke Warundi uwa ni wagumu kama walivyo Masai.
 
Aaah hhhaaa noma Sana, kuna watu wa nchi fulani wanakinga ya magonjwa Fulani Fulani, Burundi na North Korea ni mojawapo
 
Back
Top Bottom