Burundi: Kwanini Viongozi wetu wakuu wameelekeza nguvu zao huko?

Burundi: Kwanini Viongozi wetu wakuu wameelekeza nguvu zao huko?

Leo Rais Samia Suluhu Hassan anaanza ziara ya siku mbili nchini Burundi. Huyu ni kiongozi wa tatu wa juu kutembelea nchi hiyo ndani ya awamu hii ya sita. Alianza Makamu wa Rais Dr. Philip Isidor Mpango akafuata Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Nchi hii inaumuhimu gani kwetu kwa viogozi wetu wakuu kuelekeza nguvu zao huko, je soko lao ni kubwa kuliko nchi nyingine za ukanda wa Maziwa Makuu? au ni sababu za kiusalama.
Hkuna lolote ni nyumbani kwa kina Meko na Makamo wa rais
 
Kwa tozo hizi ni bora Mungu atutendee miujiza tena
Kwa style hiyo hayo maombi ya kutendewa miujiza hayatoisha, kwa sababu hata hao waombaji ni sehemu ya tatizo pia na ndipo miongoni mwao hutoka hao wanaoombewa wakumbwe na miujiza.
 
Mama anakwepa homa ya tozo mpya, huko Burundi Bora angebaki ashughulikie uchumi aisee
Cariha, Burundi ni muhimu sana kwetu, katika nchi za Afrika Tanzania ni nchi ya kwanza ambayo Burundi inatutegemea katika mahitaji na ni nchi ya 5 katika mfululizo wa nchi zinazotegemewa na Burundi. Angalia mtiririko huu;

1. China
2. Saudia
3. India
4. UAE
5. Tanzania
Hivyo ni mdau muhimu na anafaa kupewa ushirikiano ili kudumisha biashara baina yetu.
Biblia inasema "shika sana ulicho nacho"

Tunapenda kubeza kila kitu, anachofanya raisi katiks hili ni sahihi, hili la miamala sisi ndio tunatakiwa kuonyesha kuwa tumekerwa...tuweke migomo au tuandamane.

Sio kila kitu tusubiri tamko, wao wanafurahia kwani tozo litatimiza malengo yao ya kisiasa. Katika hili kuna wanasiasa watafikia malengo yao aidha positive au negative kama ifuatavyo:
1. Huenda washauri wa raisi wanalenga kumkwamusha, hivyo mambo yakienda kombo watakuwa wamefanikiawa au

2. Endapo raisi na serikali wakalisimamia hili vizuri na mambo yakabamba basi kwa matokeo chanya atakuwa amejiweka nafasi muhimu.

Tuchukue hatua sisi au tusubiri matokeo ni juu yetu.
 
Hatuuzi litu kwasababu njia za mawasiliano kule ni duni barabara reli n.k ujinga wa viongozi kupeleka vipaumbepe kusiko sahihi. Inashangaza SGR ilikuwa inapelekwa kwa kagame nchi moja walati burundi kiuahilisia unakua umegusa mkoa wa kigoma na nchi ya DRC
Hahah Burundi hii hii au Kuna nyingine?[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Screenshot_20210610-215406.jpg
 
Back
Top Bottom