Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Shirika la Human Rights Watch limesema katika ripoti yake iliyotolewa leo kuwa maafisa wa serikali na wanachama wa kundi la vijana linaloogopwa la chama tawala wanaitisha pesa kwa lazima za uchaguzi mkuu unaokuja
Dhulma zinazohusiana na ushuru wa uchaguzi wa mwaka 2020 nchini Burundi, zinaonyesha kampeini ya chama kinachotawala (CNDD-FDD) huku kundi la vijana na maafisa wa serikali wakikusanya ''mchango wa hiari'' kutoka kwa raia. Shirika la Human Rights Watch limefichuwa kuwa watu wamelazimishwa kulipa ada mara kwa mara ama hata zaidi ya kiwango rasmi la sivyo wanyimwe risiti na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.
Kulingana na mkurugenzi wa shirika hilo la Human Rights katika eneo la Afrika ya Kati Lewis Mudge, maafisa wa serikali katika eneo hilo pamoja na kundi la Imbonerakure, huonyesha kiwango cha kuhofisha cha udhibiti wa mienendo ya watu na shughuli za kimsingi kama kununua chakula, kumuona daktari ama kupata maji. Ameongeza kusema kuwa ''Ushuru wa uchaguzi umefungua njia ya dhulma zaidi.''
Shirika la Human Rights Watch liliwahoji zaidi ya watu elfu 80 ikiwa ni pamoja na wahanga 65 wa dhulma hizo. Wahanga hao ni kutoka mikoa 13 kati ya 18 nchini humo. Agizo la serikali la mwezi Desemba mwaka 2017 liliweka michango ya kukusanywa kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na michango ya ''hiari'' ya dola 1.08 kwa familia, dola 0.54 kwa mwanafunzi wa umri wa kupiga kura, na michango ya moja kwa moja kutoka kwa mishahara ya wafanyikazi wa sekta ya umma na wazumishi wa umma.
Lakini wanachama wa Imbonerakure ambao hawana jukumu rasmi katika serikali ama katika kukusanya ushuru huo, walitumia ghasia na hujuma kupata pesa kutoka kwa raia. Waliweka vizuizi vya barabarani kukagua risiti na kudhibiti hatua ya kuingia katika masoko, shule, mabomba ya maji na huduma za usimamizi kwa wale walioshindwa kuzingatia malipo hayo.
Wahanga wanasema wanachama wa kundi hilo la Imbonerakure katika vituo vya kusambaza chakula vinavoysimamiwa na makundi ya misaada , waliwapiga watu, kuwazuia kupata chakula ama kuwapokonya chakula hicho kwa nguvu.
Rais Pierre Nkurunziza alitangaza kufutiliwa mbali kwa ukusanyaji huo wa ushuru mnamo mwezi Julai mwaka 2019 na kudai kuwa malengo yake yamefikia kutimizwa lakini akaseam wale wanaotaka kuendelea kuchanga kufanya hivyo.
Shirika la Human Rights Watch lilifichua kuwa ushuru huo wa uchaguzi bado unaendelea kukusanywa japo kwa kiwango cha chini huku kundi hilo la vijana na maafisa wa serikali wakiendelea kukusanya''michango mingine'' kwa chama hicho tawala na miradi mingine nchini humo.