Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 43,233
- 51,648
Hii nimeikuta huko kwenye majukwaa menginem imezoeleka hapa Tanzania kuyaita mabasi luxury endapo yakiwa na:
Vimulimuli kwenye roof
Taa za mapambo nje na ndani
Muziki mkubwa
Carpet
Rangi nyingi
Wheel caps
Dereva na wahudumu wamevaa tai
GARI KUWA NA CHOO PEKEE SIO KIGEZO CHA GARI HILO KUWA LUXURY
Ndugu Msomaji
Bila shaka umepata kuona magari yakiitwa Lakshari(luxury) au yakipewa hadhi hiyo. Na wengi tumezoea kuambiwa ile gari ni luxury ilee, ina choo ndani. Sasa swali ni je, kuwa na choo ndiko kunafanya gari kuwa luxury?
JIBU NI HAPANA kwanza choo sio luxury, hivyo gari(basi) kuwa na choo tu hakulifanyi basi hilo kuwa na daraja la lakshari. Kwani choo ni hitaji la msingi la binadamu. Mtu anapokwenda chooni haendi kustarehe, analazimika tu kwenda. Ingekuwa amri yake labda angependa siku nzima ipite bila kwenda chooni. Kwa hiyo choo sio anasa (luxury) au starehe, bali ni hitaji la kiutu.
Kanuni za LATRA za Usafiri wa Abiria, zimeondoa Choo kuwa kigezo cha gari kupewa daraja la luxury. Kanuni imeweka vigezo vingine kabisa vya msingi vinavyozingatiwa ili gari lipewe hadhi ya luxury. Vigezo hivyo ni vifuatavyo:
1. UPANA WA BASI Upana wa Basi usizidi Mita 2.6m
2. KIMO KWENDA JUU Kimo cha basi kisizidi mita 4.6m;
3. SITI
a) Mpangilio wa Siti uwe wa 1 by 1 au 1by1by 1
b) Siti ziwe zinawezekana kuadjasti au Kurekebishika(Kukunjika).
c) Nafasi Kati Ya Siti Na Siti Na Urefu Wa Kiegemeo
Nafasi kati ya siti na siti usipungue 780mm, na urefu wa siti kwenda juu usipungue 800mm. SIO MTU anakaa kwa kujibana bana, hawezi hata kunyoosha miguu, siti zimebanana hatari. Sasa hapo starehe inatoka wapi kama mtu hawezi kukaa kwa kujiachia?
d) Upana Wa Siti Usipungue 520mm
e) Siti Lazima ziwe na Mikanda kwa ajili ya Usalama
4. UWEPO WA TAA ZA NDANI YA GARI NA MWANGA
Basi liwe na taa walau tatu kwenye korido na pia kwenye kila siti ya abiria iwepo taa inayoonesha siti.
5. UWEPO WA MFUMO WA UPOOZAJI HEWA(Air Conditioning)
Basi lazima liwe na AC au ukipenda mfumo wa upozaji hewa unaofanya kazi vizuri. Yaani abiria wakiwa ndani ya gari wapate kiyoyozi.
6. TV: Gari lazima liwe na TV walau Saba(7)
7. REDIO Basi lazima liwe na redio ya sauti.
8. KIPAZA SAUTI: Basi lazima liwe na kipaza sauti (microphone)
9. PAZIA: Basi lazima liwe na mapazia dirishani.
11. HITA: Basi lazima liwe na hita ya kuchemshia maji.
12. FRIJI: Gari lazima liwe na friji.
13. VINYWAJI: Gari lazima litoe huduma ya vinywaji baridi kwa ajili ya kuwaburudisha abiria.
14. VTS: Basi lazima lifungwe kifaa cha kufuatilia mwendo, yaani VTS.
15. CAMERA: Basi lazima liwe na CCTV camera ndani.
16. SKRINI YA SPIDI: Ndani ya basi lazima kuwe na skrini inayoonesha mwendo wa gari.
Iwapo basi litakidhi vigezo hivi basi litapewa hadhi ya LUXURY, na likishakuwa na hadhi hiyo, Mtoa huduma anaruhusiwa kujipangia nauli yeye mwenyewe bila kusubiri kuidhinishiwa na Mamlaka.
Ni Imani yangu umeongeza uelewa.
RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote
See less