Mikono yenye Sugu
Senior Member
- Jul 1, 2020
- 133
- 215
Naam, siku zinazidi kusonga na zimebaki siku 26 Watanzania tupige kura kuchagua madiwani, wabunge na Rais. Sio siku nyingi, japo pia sio chache. Kwa jinsi mambo yanavyokwenda kuna kila dalili kuwa kuna mtu timu yake inalemewa na anachezewa nusu uwanja.
Kampeni zilianza vizuri huku vyombo vya dola, hususan jeshi la polisi, vikionekana kusimamia wajibu wao ipasavyo. Tume kwa upande wake haikupata kueleweka vizuri tokea ianze kutekeleza zoezi la engua-engua ya wagombea wa upande mmoja huku wengine wakiwa salama salimini.
Kama vile haitoshi, tunaanza kuona tume ikichukua wajibu wa Afisa Itikadi na Uenezi wa chama chetu. Hiyo sio dalili nzuri. Jeshi la polisi nalo limeanzisha manyunyu ya maneno. Haifai mambo kuwa hivyo.
Wakati hayo yakijiri, tayari balozi wa USA hapa nchini na mwanasheria wa mmoja wa wagombea wameshahadharisha juu ya mwenendo usioridhisha katika kuelekea siku ya uchaguzi.
Naamini dhamira ya kuwa na uchaguzi wa amani ipo na haifai kuvurugwa kwa namna yoyote. Chama changu hakina sababu ya kuweweseka bali kujikita kuzitafuta kura za vijijini ambako siku zote ndiko uliko mtaji wetu. Kwa Watanzania wanaotafakari vizuri pasi na ushabiki wanaziona kazi njema zilizofanyika na watatupa kura. Siku zote ukweli huishi kwenye vilindi vya mioyo ya watu. Hatuhitaji kupendelewa au kubebwa.
Chama changu kisitatufute kujitia doa kwa kulazimisha au kushawishi mamlaka za usimamizi wa uchaguzi kutupendelea. Hao ndio watatuharibia na kupelekea taswira ya nchi yetu kuharibika na kujikuta tunatumbukia kwenye shimo la nchi zinazowekewa vikwazo na mataifa mengine ikiwemo bidhaa zetu, hasa mazao ya kilimo, zikikosa soko kutokana na vikwazo.
Busara na hekima vituongoze na imani yangu ni kwamba tutavuka salama.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.