Busara itumike matumizi ya barabara za mwendo kasi. Kuzuia polisi na vyombo vya dola kunaweza kuleta athari katika kudhibiti uhalifu

Busara itumike matumizi ya barabara za mwendo kasi. Kuzuia polisi na vyombo vya dola kunaweza kuleta athari katika kudhibiti uhalifu

Kwa foleni ya magari iliyopo Dar es salaam na wakati mwingine barabara za mwendo kasi zinakuwa wazi sioni kama ni sahihi kwa kuzuia polisi au watumishi wa vyombo vya dola ambao wanauharaka wa kwenda kutimiza majukumu ya kudhibiti uhalifu.

Piga picha utafakari kuna ghasia au benki imevamiwa mahala popote Dsm na kuna foleni , askari wakitaka kuchepuka ili kutumia barabara ya mwendo kasi kudhibiti uhalifu ni kosa? La hasha.

Tusipende kufanya maamuzi kisa tu kuna kelele za wapuuzi wachache huko Twita ambao hujiona wajuaji wakati ni wapuuzi tu

Idugunde nikiwa Kayenze Mwanza.
POLISI ni wasimamizi wa Sheria, wasiruhusiwe kuvunja Sheria baas!!!!

Mbona treni ikipita Huwa hawakatizi hata kama Wana haraka na taarifa za kiinteligencia?????
 
Wakati mwingine inabidi tufikirie nje ya box. Abiria wa mwendokasi wame sacrifice kutumia usafiri huu. Lakini inaonekana watumiaji wengine wana uhitaji. Kama ni hivyo, iwekwe tozo kwa wale wote wanaotaka kutumia hizo barabara.

Kwa waliotembelea miji ya wenzetu kama Chicago hivi, kuna express way kwa wasafiri wenye uhitaji Kama huo
 
Nchi ngumu sana

Kwa wale wenye exposure kutoka kwa wenzetu wanacheka tu hiiiiiiiii

Ova
 
km kuna umuhimu huo basi sheria za matumizi ya barabara hizo zifanyiwe amendment ili hilo unalosema liwezekanae otherwise sheria ni sheria, hii nchi kuna watu hawajui km taasisi za usalama nazo zinatakwa kufuata sheria, hilo ni tatizo kubwa
Kweli yanayojiri hivi sasa yanafurahisha. Hivi kweli majeshi yetu (JW, Polisi, Zimamoto na Uokoaji, MAGEREZA, Uhamiaji) yanapopita mabarabarani yakiwa kwenye dharura inabidi hivi sasa sisi wananchi tuwasimamishe na tusiwapishe hadi tutakapowahoji watufahamishe ni dharura gani wanayoenda kushughulikia ndipo tuwaruhusu wapite?
Kweli kabisa tumefika huko? Sasa naamini kuwa Uhuru ukipita kiasi....😳🤔
 
Umeshaona kwenye zingine zenye barabara km hizo wanafanyaje?, dharura inajulikana na taasis husika zinatakiwa na sheria kuwa na ving’ora kuwaalert watumiaji wengine wa barabara kinyume na hapo sheria za kawaida lazima zifuatwe, sisi waafrica sijui tunamerogwa nn maana bado tuna mawazo ya kijima,
 
Back
Top Bottom