Busara kidogo inahitajika katika hili

Busara kidogo inahitajika katika hili

Relax mkuu. Kuna vitu sio vya kuchukulia serious namna hii. Umewaza mpaka habari za incest, that's too much imagination for such an ordinary storyline!
Hiyo ndio dhima kuu ya ubongo, kufikiria. Ndio maana nimesema fikra zangu hizi zinaweza kua si sahihi kutokana humu tu watu wa historia,tamaduni na mila tofauti kutokea maeneo tofauti ndio maana wengine humu ni rahisi kumwambia mzazi wake kua "Nakupenda Baba" jambo ambalo Kwangu au kwetu ni kitu cha ajabu sana ajili ya mila na tamaduni za kwetu.

But kwa zile mila Common za muafrika sidhani kama ni vyema kumuita baba yako kua "This man,Huyu Mwanaume, yule Mwanaume". Mbele ya watu wazima utaonekana una utovu wa nidhamu na heshima.

Je wewe binafsi unaweza au unaona kwako sawa ukiwa mbele ya marafiki au ndugu zako unamu-Address mama yako kwamba "Yule mwanamke, huyu mwanamke, That woman, n so so so...? Unaona kwako hilo ni sawa kulifanya.??

Lakini pia bado naweza kua sipo sahihi kwa hili nililoeleza hapa, so mtakaonielewa vibaya mnisamehe.. Being Right is relative...I might be right because I fed your Ego and I might be wrong coz ain't fed your Ego

Btw ningependa mjadala wa kuhusu Kumuita mzazi huyu au yle uishie hapa maana sio lengo kuu la mtoa mada. Tujikite sasa katika mada!
 
Una kesi kama ya shosti angu mmoja ila yeye aliamua kusimama upande wa Mama yake na Baba mlezi. Huyo Baba mzazi muache alalamike weee atachoka mwenyewe kamwe usije umiza waliokua nawe kipindi kigumu na cha furaha.

Hawa jamaa wa hit and run ndo kawaida zao hizo. Anakimbia huku akijua kuna mimba au mtoto katelekeza anabaki kujipa matumaini atanitafuta akikua.

Ukisogeza ukaribu zaidi kituo cha pili kitakua kutembeleana,leo atataka uende huku kesho kule kesho kutwa pale.

Muheshimu tu kama mmoja wa wazazi wako.
thank you so much dear Numbie..!!
 
Ni Kazi sana kutengeza Bond kwa sasa.

Bond inatengenezwa toka mtoto yuko tumboni, anazaliwa.
Pale analia anabebwa na mikono ya Baba. Anamkojolea, anakua, anachezea viatu vya Baba, anamchafua, anaanza shule, anachapwa kisha anabembelezwa. And so on...... Na hakuna shortcut

Baba yako ali- mess up, asitegemee mambo yatakuwa sawa tuu.

Kwa upande wako wewe hauna kosa, usijilazimishe kumlidhisha.
Shukrani sana Genuine Man..!
 
Naandika applications nikimaliza nakuja inbox tuone tunatackle vipi hii incident
 
Natumaini unaona hizo sehemu nilizoBold na kuweka strikethrough
-
Kwa tamaduni zetu za kiafrika mtu ambae unamuheshimu kama mzazi hutakiwi kumu-Address kama ulivyofanya hapa, kwa muono wangu sidhani kama inaleta picha nzuri kumuita baba yako mzazi au mlezi "Huyu Mwanaume" hilo ni jina analoweza kuita mama yako pekee. Otherwise Ukifanya kama ulivyofanya hapa wengine wanaweza kuhisi kuna hali ya incest kati yenu. Maybe ndio maana nae inakua rahisi kukuita "Toto langu"

I'm so sorry for saying this to you I might be wrong too but my point is pinned to the fact that the way you address your father figure is not Healthy. Change!!!!
______
Rolling to the main topic!!

Kuna Father na Daddy, Father anatia mimba hajali Mtoto atakua vipi na kuishi vipi...Daddy anatia mimba na kujali kiumbe hicho alicholeta duniani kwa "Kuwepo" pembeni ya kiumbe huyo siku zote. Kwa maelezo ulivyoeleza huyo aliyekuzaa he was your father but wasn't your Daddy. Anachokifanya ni kutaka kula mavuno ya shamba ambalo hakulipalilia, jambo hili Hata Mungu kakataza. Maana anasema...

Mathayo 25:24,28,30
[24]Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
[26]Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
[27]basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
[28]Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
[30]Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Btw Kwakua hatujajua kisa cha mzazi halisi kukutelekeza basi Siwezi mlaumu. Ila cha msingi ongea na mama yako akupe kisa chote cha baba yako kukuacha kisha msikilize na baba yako pia upande wako then wewe mwenyewe utaamua cha kufanya. Choose wisely

Obvious naamini baba yako anachotaka ni kupata recognition ya kua wewe ni mtoto wake if so basi mpatie. Mjulie hali hata kwa simu mara moja moja mtembelee, ila mapenzi kwa baba mlezi usipunguze kamwe.
thank you Vinci,
Ila haupo sahihi kufikiri unachofikiri, what I feel for that man is unexplainable, na nina haki ya kumuita vyovyote ambavyo sitendi dhambi..!

thank you once again, ushauri wako ni mzuri sana na nitaufanyia kazi pia..!
 
Anataka kuvuna asichopanda
Sasa wewe hiyo bond utaitoa wapi, mtakuwa mmeipanda lini, au ndo damu nzito kuliko maji.

Muhimu ni kumsamehe na kumheshimu basi
Hayo mengineyo anafosi tu kwa sababu ya guilty
Shukrani sana mpendwa..!
 
My dear huyo ni sperm donor sio baba akao anaona haya na kuumia kwa kua umelelewa vzr umekua vzr mama na mwanaume mwingine wameplay part vzr usije kumuumiza aliyekula nawe toka utotoni rafiki,jus mchukulie kama wengine.Jiulize ungekua jambazi au huna direction angekutafuta?!!achana nae

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
Kumuumiza yule baba, ni dhambi ambayo sina pa kuitubu.!
Shukrani my dear Rey..!!
 
Yaani umeshauri kitaalam sana big up watu kama wewe ni wachache! Mtoto anaweza kulishwa sumu ya maneno na akajenga chuki bila kujua upande wa pili
Upo sahihi ila hakuna sumu yoyote nimelishwa, the fact that he won't there ni sumu niliyokula mwenyewe tayari..!
Ahsante.
 
Relax mkuu. Kuna vitu sio vya kuchukulia serious namna hii. Umewaza mpaka habari za incest, that's too much imagination for such an ordinary storyline!

Back to the topic, nimeona vitu kadhaa:

- Baba mzazi hakufanikiwa kupata mtoto wa kike huko aliko. Ndugu mleta mada, do you really think the old man angekutafuta kama huko aliko angepata mabinti kadhaa? Hata usinijibu hili swali.

- Baba mlezi hajui kama unawasiliana na baba mzazi. You're about to hurt that old man. Sisi wanaume tunakuaga very territorial. Once we have what we consider to be family, haturuhusu another man aingilie chain of command and how we're running the show. Mlezi akigundua baba mzazi is back, and you're sneaking behind his back, ataumia kinoma. Ni either umwambie mwenyewe, au uache ku-hangout na upande wa baba mzazi.

- Hakuna bond kati yako na baba mzazi, zaidi ya baiolojia iliyokuleta duniani. Umekua na undugu na upande wa baba mlezi. Brothers, sisters na wengineo, they all consider you one of their very own. Huko kwa baba mzazi hautaweza kutengeneza bond mpya, na kama ukiweza kuna mahala utavunja kwa ndugu zako wa upande wa baba mlezi. Pick your side wisely sweetheart!


Kwa upande wangu, undugu sio kushare damu. Undugu ni nani yuko na wewe through thick and thin. Nani anaguswa na shida zako? nani anaumia ukipitia magumu? Binafsi, kuna washkaji tu nawathamini kuliko "ndugu". It's because they've got my back when shit goes down!

Nashauri ukae na baba mzazi, umpe ukweli. Mwambie nakutambua mzee, and I do respect you. Ila hatuwezi kua na bond like family. I already belong somewhere else. Kuna watu wamenikuza like one of their own, itakua ngumu kuswitch sides kwa sasa. Tuendelee tu hivihivi.

Ukimaliza hapo, rudi kwa Baba mlezi umpe picha nzima. And maybe, muulize anashauri nini. It will make him feel better, kuliko kukaa kimya huku akiwa anajua kinachoendelea.

NB: kumbe mleta mada uko na light skin sio? Uko na kapicha tuone?
thank you Smart Ghost, you real are the best..! Nitafanyia kazi ushauri wako..!!
 
duh! haya mambo yapo sana kwa sisi tunaoishi na masingle mother, ila pia unatakiwa kuelewa kuwa huyo baba ako mzazi aliachana na ur mumy kwa7bu zipi! usukute labda alifumaniwa, au usikute labda huyo baba ako mzazi ndiye aliyeharibu mahusiano yake kayi ya baba mlezi na mama ako
Baba mwenyewe alisema ulikuwa ni ujana na anajutia, hivyo it was never My Ma's fault..!
 
Lil sis don't stress yourself; Wala hata usiwaze huyo baba yako anajisikiaje; sio shida zako hata kama umemsamehe.

Baba yako ni mtu selfish; wakati wewe unamuhitaji kwenye maisha yako; yeye hakuwa tayari. Muda huu yeye anakuhitaji wewe na anakulazimishia; sio sawa.

Ukweli ni kwamba sio kila mwanaume ni baba. Kuna watu wengi waliolelewa na baba zao; lakini hicho alicho/anachokupa baba yako mlezi; kuna millions of people hawajawahi kuki_experience. Mshukuru huyo baba yako mlezi sanaaaaa. Hujapata ombwe/ trauma kwa sababu ya kutokulelewa na baba; kwa sababu yeye aliamua kuwa baba ambaye hukuwa naye. Mimi ninajua umuhimu wa uwepo wa baba kwenye maisha ya mtoto wa kike; kwa kukukubali wewe na kukufanya mtoto wake uuuh; kitu kikubwa mnoooo, ni neema.

Tena mama yako mmmh basi tu; mimi binafsi ningekupa na surname ya huyo baba mlezi period; ingebaki tu damu yake kwako maana haiwezi kutolewa. Ubaba sio tu kumwaga mbegu; ubaba ni malezi. Baba ni yule anayejua umekula nini, umevaa nini, umelala wapi; anakupenda, anakujali, anakufundisha, anakuoyna, anakuwa concerned na wewe kwa Kila hali. Ukiumwa, ukiwa na changamoto yoyote; he is always there you. Huyo ndiyo baba na hicho kinacho-form bond kati ya mtoto na mzazi. You are an absentee parent; don't expect any bond with your child

Huyo baba yako mzazi; kaa naye kwa kina mwambie tu you are at peace with him, unamtambua kama baba yako mzazi; ila huwezi kuwa karibu naye kama anavyotamani. Ni mtoto wake kwa kukuzaa; but alishauza hiyo haki kwa mwanaume mwingine.

Nenda kamwambie baba yako mlezi ukweli wote; asije akakuona you are an ingrate. Naamini amefanya Kila kitu kwenye maisha yako kwa sababu ya upendo na sio kungoja shukrani. But kiubinadamu tu; mpe tu shukrani zake; una deni juu yake. Mpe na msimamo wako juu ya huyo baba yako mzazi. Hakikisha baba yako mlezi ana amani juu yako. Don't lose than man, don't hurt him, don't disappoint him. Make him proud; isije siku akasema "mtoto wa watu ni wa watu tu".
Big C'ssy..!
this made me cry..!
Hii pasaka nitaonana na Baba Mlezi na nitamuambia ukweli, sikuwa nimeonana naye this soon pia ndiyo sababu.!
Nazipenda hizi busara zako mno, Mungu akujazi heqma daima C'ssy..!
 
Back
Top Bottom