AFRIKA ACTIVE ACTIONS
New Member
- Oct 13, 2024
- 3
- 2
Januari 1976,huko Ethiopia,Addis Ababa, mkutano maalumu wa wakuu wa nchi za OAU uliitishwa Ili kupata suluhu ya mgogoro mzito na wa kutisha uliotaka kuligawa bara la Afrika vipande vipande.
Mgogoro huo ulikuwa baina ya nchi zilizokuwa zinaiunga mkono serikali ya MPLA chini ya Antonio Agostino Neto na zile zilizoipinga serikali hiyo.Chanzo cha mgogoro kilitokana na misingi ya itikadi za Kikomunisti (Urusi,Cuba na China) na Kibepari(Marekani na Ulaya) chini ya mwanvuli wa vita baridi.
Kwa leo hii naufananisha mgogoro huu na matatizo ya sasa ya bara letu la Afrika mathalan ya huko Afrika Magharibi(ECOWAS) yaani kati ya nchi Chad,Niger,Mali,Gabon na Nigeria, Senegal n.k.
Mwenyekiti wa mkutano huo alikuwa ni Iddi Amin wa Uganda hasimu mkuu wa Nyerere wa Tanzania.Pia katika mkutano huo kati ya nchi 22 zilizokuwa zinaiunga mkono serikali ya MPLA chini ya Antonio Agostino Neto na nchi 22 dhidi ya serikali ya Neto ilibidi wakuu wa nchi au serikali wahutubie.
Na Mwalimu Nyerere ilibidi aanze kuhutubia kama mtetezi mkuu wa serikali ya MPLA chini ya Neto Ili baadaye upande wa wapinzani wa serikali ya MPLA chini ya Neto nao wahutubie. Mambo yakawa kinyume chake, Iddi Amin akapindua ratiba Kwa kuruhusu wapinzani wa serikali ya MPLA chini ya Neto kuanza kutoa hoja zao dhidi ya serikali ya MPLA.
Rais Kenneth Kaunda wa Zambia ,rafiki na jirani wa Mwalimu Nyerere akapewa rungu la kutoa hoja za kupinga serikali ya MPLA.
Rais Kaunda alihutubia Kwa hisia kali za kuipinga serikali ya MPLA pamoja na kuzipinga nchi za Urusi na Cuba na kuungana na wapinzani wa serikali ya MPLA na kuashiria kutokea kwa mpasuko mkubwa miongoni mwa wanachama wa OAU.
Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kutoa hoja za upande wa wanaoiunga serikali ya MPLA, mambo yakawa kinyume tena.Mwalimu Nyerere hakutoa hotuba!Kwanini?
Kumbuka zama hizo washauri wa Mwalimu Nyerere,Waziri wa Mambo ya Nje(Ibrahim Kaduma),Salim Ahmed Salim (Balozi,UN),Katibu wa Rais(Joseph Butiku) ,Katibu Mahsusi(Joan Wicken) na wengineo waliambatana na Mwalimu Nyerere katika mkutano huo.
Hivyo Mwalimu Nyerere aliamua kutohutubia yaani kutoa hoja za kuungana na serikali ya MPLA Kwa sababu ya masilahi mapana ya bara la Afrika.Hiyo yote ilikuwa ni kunusuru kuvunjika kwa OAU(per excellency)
Heko Mwalimu Nyerere! Leo hii Umoja wa Afrika (AU) pamoja na misukosuko (challenges) yote inayotokea ungali upo!Huyo ndiye Mwalimu Nyerere Mwanajumui wa Afrika (The Pan-Africanist) kutoka Tanzania.