Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Nimeitazama video moja ya hayati mchungaji Myles Munroe akiwaongelea wanasiasa wa dunia hii. Nikatamani hawa wa kwetu waisikilize ili waondoke na chochote kitu kitakachowasaidia katika wito wao wa siasa. Ni video yenye kutafakarisha kwa kina juu ya maisha mazima ya mwanasiasa.
Anasema kwamba hata siku moja usiamini kwamba mwanasiasa ni kiongozi, kwa sababu mfumo tulionao unatengeneza wanasiasa hautengenezi viongozi. Anasema unaweza kuwa na mwanasiasa asiyejua chochote kuhusiana na uongozi na akawa anakuongoza.
Mwanasiasa siku zote anachokiwazia ni uchaguzi mkuu ujao na hiyo ni sababu hawezi hata siku moja kuwa kiongozi. Kwani kiongozi anaguswa na hatima nzima ya pale anapopaongoza. Kiongozi anahofia kizazi kijacho kitakuwa vipi na kitafanya nini ili kifanikiwe.
Na hapa kwenye suala zima la maono ndipo siasa inapopungukiwa kuilinganisha na uongozi. Uwezo wa kuguswa na kesho ya eneo husika upo katika nafsi za viongozi haupo katika nafsi za wanasiasa.
Huwa haiwi ni ajabu kuona kila kinapofika kipindi cha kampeni mwanasiasa anakuwa tayari hata kutengeneza fulana zenye picha ya mgombea kifuani na atapita kila nyumba akizigawa tena bure, kinachomtesa nafsi yake kwa muda huo ni hiyo kura yako tu na sio kingine chochote. Mwanasiasa siku zote haja yake ni yale mamlaka na utukufu wote unaoambatana nayo, haguswi na kesho ya wanaomzunguka wala hatima ya maisha ya wajukuu zake, yeye ni leo na kesho mpaka mamlaka yake yatakapokoma kwa mujibu wa katiba au taratibu za kiuongozi zilizopo.
Uanasiasa siku zote unapungukiwa kwa kuulinganisha na uongozi. Haishangazi mpaka leo mitandaoni kuna kuwa na zile habari fupi fupi za Mwalimu Nyerere na hotuba zake za miaka ile ya 1960 mwanzoni mpaka mwishoni. Kinachowafanya watu wazitafute hotuba zile ni sifa ya uongozi inayopatikana mle. Kwamba maneno ya kiongozi siku zote huwa yanao uhai, yanagusa maisha ya mtu moja kwa moja na hatima yake hapa duniani. Uongozi haupungukiwi ubinadamu, haupungukiwi ile hali ya kutaka kubadilisha maisha ya watu kwa ujumla wao.
Uongozi huenda pamoja na ushawishi wa kimaadili, nakumbuka Mwalimu Nyerere alivyoweza kufanana na yale aliyokuwa akiyaongea majukwaani. Unauona msafara wake ukielekea Msasani na njiani anawapungia anaowaongoza kupitia kioo cha gari, hakuweka ukuta kati ya anaowaongoza na yeye muongozaji. Alipotaka kupanda maua sehemu fulani hakuweka kitamba chini ili suruali yake isichafuke, alikuwa tayari kuchafua suruali yake wakati wa kumwagilia maua kwani alijua suruali sio kitu itakwenda kufuliwa tu. Huo ndio uongozi, ni kujishusha siku zote.
Nasoma sana humu JF namna watu wanavyolilia kwa nguvu katiba mpya, ni wazo linalokwenda na wakati husika. Tatizo linabaki katika tofauti ya kiongozi na mwanasiasa. Je Katiba mpya itaweza kututengenezea viongozi waonyesha njia au tutaendelea kuwa na wanasiasa wanaokuwa msingi wa kuzaliwa kwa wapambe wa kila aina (Chawa) na siasa za kila aina za upambe na utapeli?. Kenya wanayo katiba mpya lakini pia wanao wanasiasa kina Ruto na wapigaji madalali wengine wengi wa hadhi ya kimataifa.
Ningependa sana kuiona Tanzania ikiwa na viongozi wengi wenye uhuru wa fikra, wenye uwezo wa kujitambulisha katika ubinadamu wao ulio na nia ya kugusa moja kwa moja maisha ya vizazi hata vinne mbeleni. Sio hawa wenye tabasamu mwanana kabisa lakini ni wabinafsi na wenye kuabudu siasa za makundi.
Munroe aliaga dunia tarehe 9 Novemba 2014 akiwa ameishi duniani kwa miaka 60, ujumbe wake upo hai mpaka kesho ukitupatia changamoto za maana.