Nakumbuka walikuwa na zoezi moja hivi unapanda juu ya mteremko alafu unaserereka na kichwa kwenye mawe yaliyoko chiniEeh bwana ilikuwa hatari sana.
Mimi nilikuwa napenda yale madongo wanayopeana wakati wa game.
Wa vijijini wakiwatuhumu wa mjini kuwa ni warembo/walaini kama watoto wa kike, wa mjini wakiwatuhumu wa vijijini wachafu na ushamba wao.
Bila kusahau mazoezi makali ya Bush Stars....daah!
MAPUNG'O hakuwa kwenye SANI alikuwa kwenye Gazeti la Bongo ....(?) ambalo lilikopi vitu vingi vya SANI baada ya SANI KUPOTEA MTAANI ....MSHAMBULIAJI HATARI wa kwenye SANI alikuwa MZEE Meko ....peke yake ndiyo alikuwa anavaa shati kati ya wachezaji Bush Stars na Ukimuondoa Golikipa MADENGEMapung'o japo alikua ni mtu wa bata sana.. Jamaa alikua hatari sana mbele ya goli.. Nakumbuka aliwahi kusajiliwa uarabuni kutokana na uwezo wake uwanjani.
kuna mtu anakumbuka first eleven....ya timu hizi...
mimi namkumbuka Madenge tu mzee meko wa bush stars
na mtangazaji sukununu...
Mapung'o alicheza hadi Chelsea kama sijakosea afu njumu zikawa zinamshinda.
Kacheza Chelsea wewe kipindi hicho ndo imetoka kuchukuliwa na bwana Roman,muulize Njitap au Crespo watakuambia.😀😀Alichezea Madrid maana kipindi icho chelsea haikuwa na nguvu kama leo
Hakafu wale wanawake waliokuwa wanawatengea ugali sasa ni balaaKuna mechi moja halftime mabush walipiga ugali wakashushia na togwa. Jamaa walikuwa watata sana!
Hata mm nilitaka kuuliza.. Nilikua namuheshimu sana huyu jamaahivi the boss aliendaga wapi?
Duuh..Nakumbuka walikuwa na zoezi moja hivi unapanda juu ya mteremko alafu unaserereka na kichwa kwenye mawe yaliyoko chini