Habari zenu wana jamii. Nimekua nikitafuta fund kwa muda mrefu nikabahatika kukutana na kampuni ya SYRIA inayojulikana kwa jina la (HAROUN HOLDING COMPANY) C.E.O wa kampuni hii amejitambulisha kwangu kwa jina la E.H Haroun al Assad. Baada ya mazungumzo nae akanitaka nimtumie business plan ili aweze kuni fund , baada ya kumtumia alinijulisha kua ameamua ku fund hiyo project yangu kulingana na masharti aliyo nipa. Baada ya hapo akaniuliza kama nipo tayari kufuata masharti niwasiliane na mwanasheri ambaye ni Managing partner wao. Alinitambulisha kuwa jina la mwanasheria huyo ni Dr Nahel Al Masree esq. Baada ya kuwasiliana na huyo lawyer akanitaka nimtumie personal information zangu pamoja na adress yangu na Id ndio aweze kunijulisha cha kufanya. SASA NDUGU ZANGU mimi bado sina imani na hawa jamaa kama ni matapeli au hivyo nashindwa kuwatumia maelezo yangu binafsi. SWALI NI JE kuna mtu yeyote hapa anajua kuhusu hiyo kampuni H.H.C? Naombeni msaada