Business/investor partner in lubricants importation

Business/investor partner in lubricants importation

Pohjois Haaga

Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
47
Reaction score
16
Naamini penye wengi hapaaribiki neno. Nimepewa haki za kusambaza premium brand lubricants kutoka bara la Ulaya kwa soko la Tanzania na Afrika Mashariki na Kati. Hii brand ni kati ya zilizo bora sana barani Ulaya.

Mimi Mbongo lakini nimekaa nje kwa muda mwingi ila kwa sasa nipo nipo sana . Nahitaji mtu wa kushirikiana naye kwenye biashara hii mwenzangu huyo ingekuwa vizuri awe ana ufahamu wa biashara haswa wa hapa Tanzania(maana mi mtandao wa kijamii mdogo hapa nyumbani), uwezo au ufahamu wa jinsi ya upatikanaji wa tenda za makampuni na serikalini, na mtandao wa kutosha kwenye biashara. Mwenye nia au maswali au msaada wowote kufanikisha hili naomba ani PM twende mbele.

Natanguliza shukurani
 
labda nikuweke sawa nini tz na afrika inataka.

ulizia teechnology inayotumika kutengeneza hizo lubricants uilete hapa bongo tutengeneze bidhaa tujiuzie wenyewe.

mambo ya kuuza ready made products za ulaya ni kudidimiza uchumi,mali ghafi zetu kuharibika ,kudidimiza thamani ya shilingi.

sasa watu wana mitaji na connection nzuri ya kupata mikopo mikubwa tu bank ila idea iwe ni kutengeneza hapa ndani kuuza hapa na ikiwezekana kuuza nje. ndio mchina pia anavyofanya anajifunza technolojia sio uchuuzi wa kuuza bidhaa
 
Najua point yako lakini naona umekurupuka watu wanalinda teknolojia zao na hata wakikupa hutaweza kufanya wanachofanya wao bila kujizatiti. Tutafika huko lakini sio kwa kukurupuka Wachina si wenzetu wametoka mbali sana. Anyway kwa sasa ipo fursa hii.
 
Hzo products z inaitwaje na bei yake ipoje?
 
Mkuu labda sijakuelewa,
Rasimali pesa wewe unayo,ila unachotafuta ni rasilimali watu ambaye ana connection nzuri ya makampuni na serikali?
Labda ungeweka wazi kidogo,tunaweza kufanya jambo hapa.
 
Mkuu labda sijakuelewa,
Rasimali pesa wewe unayo,ila unachotafuta ni rasilimali watu ambaye ana connection nzuri ya makampuni na serikali?
Labda ungeweka wazi kidogo,tunaweza kufanya jambo hapa.

Pusha la Magogoni, tunafuta rasilimali zote kwa maana pesa na watu.
 
Back
Top Bottom