KERO Busisi - Kigongo kivuko kimoja ndicho kinafanya kazi na kupelekea usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa huduma hiyo

KERO Busisi - Kigongo kivuko kimoja ndicho kinafanya kazi na kupelekea usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa huduma hiyo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Anordynho

Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
6
Reaction score
3
Naomba Serikali iangalie kuna changamoto katika kivuko cha Busisi - Kigongo ambapo kuna vivuko vitatu yaani MV Mwanza, MV Misungwi na MV Sengerema lakini kwa sasa kivuko kinachofanya kazi ni kimoja tu vingine vibovu.

Hali hii inasababisha foleni kubwa sana ya magari ambapo athari yake ni kupoteza muda, rushwa kwa baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri, pia kupunguza route za magari hasa ya abiria.

Unakuta gari linalopaswa kwenda route 4, kwa sababu ya foleni linaenda route 2 pekee.
BUSISI.jpg

Tunaomba Serikali iangalie hilo.

Ufafanuzi wa TEMESA~ TEMESA: Kivuko kimoja (Kigongo-Busisi) ndio kina hitilafu vingine vinaendelea na huduma kama kawaida
 
Daraja la magufuli linahujumiwa....asiyetambua kero inayopatikana hapo kivukoni utamwona na comment za kijinga but ukweli abiria wanateseka sana
 
Hali ni mbaya sana, leo tarehe 17/2/2025. Nimefika kivukoni saa tatu na nusu asubuhi mapaka sasa saa sita na dakika 10 kivuko kimevusha mara moja tu. Kivuko chenyewe kimoja kinapakia na kusubiria muda mrefu na kikianza safari ni mwendo wa kinyonga.

Vile watumishi wa Temesa wameona chenji shilingi mia ni posho zao. Shilingi mia moja chenji hairudi. Si ni bora kama coins za shilingi mia hazipo fanyeni nauli kwa abilia iwe mia tano, ili pesa iende serikalini kuliko kuishia mikononi. Can you imagine pesa kiasi gani wanatengeneza kwa siku kwa maelfu ya abiria wanaoacha hizo chenji? Ni kama vile hakuna uongozi na TAKUKURU sijui wanafanya kazi gani?
 
Back
Top Bottom