Busuness partner anahitajika haraka!

Busuness partner anahitajika haraka!

John L. Mihambo

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
526
Reaction score
177
Wakuu kitu kizuri ule na wenzako! Tuna Kampuni ya masuala ya "Technologies & General Supply", ni Limited Company by shares. Hadi sasa ina Wakurugenzi wawili tu!
Imesajiliwa kwa taratibu zote za kisheria tangu mwaka jana mwezi August pale Brela, na baada ya kukamilisha nyaraka nyingine muhimu ilianza kazi rasmi mwezi Novemba mwaka jana (2013), kule mkoani Tabora, wilaya ya Urambo. Imepanga nyumba nzima, mtaa wa boma village, barabara ya salama.

Kampuni imesajiliwa kufanya biashara mbali mbali (za kiteknolojia na masuala mengine mbali mbali kama vile usambazaji wa bidhaa, usafirishaji, utalii, madini, kilimo, ujenzi, ukandarasi, ununuzi wa mazao n.k) popote pale nchini. Kwasasa tumejikita katika maeneo machache sana kutoka na changamoto za mtaji kutokuwa mkubwa sana, kwahivi tuna karibisha partnership na kampuni yeyote ile ama mtu binafsi tutakayeweza kushirikiana naye katika maeneo mengine ya kibiashara!
(Unaweza pia kutembelea ukurasa wetu wa facebook ukajionea baadhi ya shughuli tunazozifanya kwa sasa)

Kwa mawasiliano zaidi; 0755 732 981 /0784 324 102
Barua pepe; info@mihambos.com
Tovuti; Mihambos

Karibuni Sana.

(Mods please, naomba u edit Title yangu hapo juu, ni Business Partner wakuu!)
 
Sasa hivi mna biashara ipi ambayo inaendelea?

Mnazo tax returns ambazo filed ki sheria?
Kwasasa tunaendelea na ujenzi wa mabanda ya kisasa ya kufugia nyuki, kwa NGOs zilizoko katika mradi endelevu wa uhifadhi wa misitu ya miombo, wilaya ya Urambo na Kaliua
 
Kama uko committed tuwasiliane kwenye civil/building works. Baada ya matokeo njoo tena JF uwape mrejesho. Twende PM kwa mengi zaidi.
 
Mmeshawahi ku file tax returns toka muanze shughuli zenu? kama ndio, unaweza nitumia copy kwa email?
Yes, utakapokuwa tayari kuingia kwenye ubia utapata nafasi ya kupitia nyaraka zote muhimu kupitia mwanasheria wetu!
 
Yes, utakapokuwa tayari kuingia kwenye ubia utapata nafasi ya kupitia nyaraka zote muhimu kupitia mwanasheria wetu!

Dah ntaingia kwenye ubia bila kuona tax returns zenu mnazo file brela? tena ilitakiwa hata nisikuulize niende brela nikatazame, nimefanya uungwana kukuuliza na kuondosha ucheleweshaji ili nikupe majibu kama yes ntaingia ubia au no sitoingia ibia.

Ntaingia ubia hewa?
 
Wewe unataka kuingia ubia au unataka kujua Kama kampuni inalipa kodi or not,sijakuelewa Hapa Faiza
Mimi nimeshindwa kabisa kuelewa lengo lake hasa! Sijajua yeye amesimama kama nani? Kampuni. Sole proprietor ama mdau binafsi?
Records zake zimekaaje? Anyway, dada Faiza kama unahitaji data zote hizo hapa siyo mahali pake, tunaweza kufanya utaratibu wa kuonana kibiashara zaidi tukiwa na Mwanasheria wetu!
 
Wewe unataka kuingia ubia au unataka kujua Kama kampuni inalipa kodi or not,sijakuelewa Hapa Faiza

Biashara iliyokamili inapeleka tax returns zilizokuwa verified na auditors Brela kila mwaka, haijalishi kama inalipa kodi au ina misamaha ya kodi au inapata hasara au faida.

Hiyo inanipa picture ya how organized the company is. Na inanijulisha assets zake na liabilities.

Inarahisiha kufanya decision, I have my client who is very much interested in doing business in Tabora.
 
Mimi nimeshindwa kabisa kuelewa lengo lake hasa! Sijajua yeye amesimama kama nani? Kampuni. Sole proprietor ama mdau binafsi?
Records zake zimekaaje? Anyway, dada Faiza kama unahitaji data zote hizo hapa siyo mahali pake, tunaweza kufanya utaratibu wa kuonana kibiashara zaidi tukiwa na Mwanasheria wetu!

Usiwe na hofu, mimi ni Business Consultant na nna kampuni yangu yenye wateja wengi wanao invest hapa na pale, wa ndani na wa nje.

Hilo ninalokuuliza ni jambo la kwanza kwa any interested investor kwenye kampuni iliyopo anataka ajuwe ili ahakikishe how organized you are na unachosema ndicho kilichopo na pia itampa picture ya vipi aingie nini kitamkabili akiingia au asiingie.

Hiyo ni kwa kuwa tayari umesemauna kampuni na ina biashara. Kama ungekuwa huna kampuni na biashara tayari lakini una biashara au mradi unataka kuanzisha na unahitaji partners, ningekuuliza vitu vingine kabisa na si tax returns. Ningekuuliza feasibilty study (simple one) iwe na p/l projections na iwe na ROI projections.

Nadhani itakuwa umenielewa.
 
Do not judge the book by its cover, kuwa mtazamaji hatukukuomba ushauri.

Hee! hatukukuomba ushauri, mrahii usha jimilikisha kampuni ya watu?. nawewe umekuwa mdau haya ni zaidi ya majanga.
 
Jamani ni hivi, kwasasa Kampuni imejikita katika maeneo machache sana ya kibiashara, kutokana na changamoto mbali mbali za kimtaji. Kwahivi, inakaribisha "BUSINESS PARTNERSHIP / JOINT VENTURE" na kampuni nyingine yeyote ile ama mtu binafsi atakayekuwa tayari kushirikiana nasi katika maeneo ya biashara tunayoyafanya sasa, ama katika maeneo mengine ya kibiashara ambayo bado hatujaanza kuyafanya, ama katika maeneo yote!!
Nafikiri nitakuwa nimeeleweka sasa.
 
Biashara iliyokamili inapeleka tax returns zilizokuwa verified na auditors Brela kila mwaka, haijalishi kama inalipa kodi au ina misamaha ya kodi au inapata hasara au faida.

Hiyo inanipa picture ya how organized the company is. Na inanijulisha assets zake na liabilities.

Inarahisiha kufanya decision, I have my client who is very much interested in doing business in Tabora.

hapo kwenye red ushasema kila mwaka,sasa hawa shughuli wameanza november mwaka jana,na sasa hivi april ata mwaka bado,unajua kabisa ata mwaka bado kama ambavyo umesema kwenye red hapo.

sasa huo ubishi na unachotaka kipi? watu walio serious na kazi washamtumia ujumbe.
 
Do not judge the book by its cover, kuwa mtazamaji hatukukuomba ushauri.
FaizaFoxy tax return kwa hapa bongo hebu nieleweshe dada manake na Mie nikusanye makato yangu ya mshahara mwisho wa mwaka nipate tax return? Au hiyo ya biashara is something else?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom