Buy it for Life: Tujuzane brand ama model za bidhaa zinazodumu kwa muda mrefu ili tuepukane na usumbufu wa kununua upya

Buy it for Life: Tujuzane brand ama model za bidhaa zinazodumu kwa muda mrefu ili tuepukane na usumbufu wa kununua upya

Uzi huu tujuzane bidhaa zenye viwango vya juu hasa kwa wale wasio na pesa za ziada za kubadili badili ama kwa wale wanaopenda kukaa na viru kwa muda mrefu,

Tujadiliane brand ama model za bidhaa zenye kutumika muda mrefu bila kuchoka ama kufubaa haraka, durable vyenye uwezo mkubwa wa kuhimili mazingira mengi, yaani ukinunua ni mpaka labda uje ukichoke mwenyewe ama kikiharibika huna cha kudai

Pasi ya uhakika ambayo haijachuja kwa ubora wake hapa kwetu ni phillips,

View attachment 2868879


Furniture zako jipinde chonga za mbao ya Mninga, utazitumia miaka nenda rudi hata wajukuu wanaweza zikuta

View attachment 2868518

Laptop inayodumu nunua Chapa ya LENOVO THINKPAD, hili dude utalitumia mpaka uchoke mwenyewe

View attachment 2868506

Jeans - chapa ya Levis ukiikuta hata mtumbani ibebe haraka, utaivaa sana ukifulia sabuni ya kipande

View attachment 2868708
Blender- Oraimo
Charger- Oraimo
Cm - iPhone
Earbud - Oraimo freepod Pro
Heater- Oraimo
 
Changamoto ni kuwa hizi brandi zote nzuri tunazozitaja hapa mchina anafyatua kopi zake na na ni ngumu kuzitofautisha. Mfano pasi ya phillips ukipata made in indonesia ni og ila za china uongo sana. Same goes kwa hayo ma blender and so on.
Tujuzane pia namna ya kutambua original kwenye hizo bidhaa.
 
Watu wengine mkikamata pesa shida sana, sio kila mtu ana pesa za kubadili vitanda kila mwaka, hata wewe huwezi jua kesho yako.
Wengine misifa tuuuuu. We mwenyewe uchunguze utawaona. Wengi wao hawana cha maana,hata kikiwepo ni hicho hicho. Labda wanaokilalia watabadilishwa,siyo kitanda
 
Vifaa vya jikoni km.blender,food processor,juicer na wenzake tumia NINJA
 
Back
Top Bottom