Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

Siyo kwamba Tundu Lisu hajui madhara ya matamko yake juu ya Mwl, Nyerere, amelewa sifa ya kuitwa mwanasheria maarufu, hasa hasa alivyoambiwa hivyo na Rais Kikwete.
Mtanzania halisi
Hakuna madhara kumgusa nyerere maana ameshatangulia mbele ya haki mnaogopa kwa kutoelewa tu,mwogopeni MUNGU kwa kukataa maovu maana GOD anaexist all the time kuliko kuogopa mtu aliekufa,watz vp,bado mnaabudu mizimu?
 
Mimi siku zote uwa nadhania kuwa mtu intelligent uwa anasolve tatizo kwa njia ya busara na si kuleta ubishani usio na faida na kupoteza muda....
sasa kapoteza muda gani wakati hati imeshapatikana kwa ajili ya alichosema,rais jk alishawahi kumsifia lissu kuwa yeye peke yake ni kama bunge zima?...lissu ni intelligent na INAHITAJIKA INTELLIGENT MIND KUMWELEWA LISSU
 
MKUU KIUKWELI WW NDO UTAKUWA SIO INTELLIGENT MAANA INTELLIGENTS WOTE TUMEMWELEWA LISSU.......HE IS THE ONLY TANZANIAN WHO DARED TO SPEAK THE TRUETH OPENLY,nyie mnazungumzia kiunafiki na kisirisiri
 
"Intelligence" ya mtu haipimwa kwa kuangalia wanaomuunga mkono. Inawezekana waliowengi wakawa na mtazamo usio sahihi kuhusu jambo fulani. Galileo alishawahi kuonekana kilaza kwa sababu ya kuibua mambo yaliyokuwa tofauti na mtazamo uliozoeleka lakini leo anakubalika kuwa alikuwa intelligent.
 
Mkuu,

Kwa HOJA zile NZITO za TUNDU LISSU ambazo wengi tulikuwa tunamsubiria mtu atakaye JITOA MUHANGA kuja kuziongelea ndani ya bunge hilo maalum la katiba ,nadhani TUNDU LISSU ni zaidi ya wajumbe wooote waliopo kwenye bunge la katiba!

Ni nani angeweza KUTHUBUTU kuongea yale aliyoyaongea kwa hawa WAHAFIDHINA walionyweshwa maji ya bendera!!?

HEKO TUNDU LISSU!!!

MTANGANYIKA DAIMA!
 

Mbona unaleta hoja nyingine kabla hii uliyoileta haijafika mwisho.Kweli CCM mna mambo
 
Lissu anastahili doctorate ya heshima maana ameonyesha upeo mkubwa wa kufukua na kupembua mambo kuliko midokta na miprofesa iliyokaa bungeni kutoa hoja za kitoto
 
Kumbuka mtu anayebaki kwenye historia na aliyebaki na maisha yaliyopo aiwiwe mambo mengine ya baadae basi mtu huyo ajue hawezi pata maendeleo kama wewe, kumbuka phylosophers wengi wamepita lakini bado tumeainisha mapungufu yao sasa sembuse baba wa taifa? Y yeye dont be stugnant in idiology
 
Kumbuka mtu anayebaki kwenye historia na aliyebaki na maisha yaliyopo asiwiwe na mambo mengine ya baadae basi mtu huyo ajue hawezi pata maendeleo kama wewe, kumbuka phylosophers wengi wamepita lakini bado tumeainisha mapungufu yao sasa sembuse baba wa taifa yeye? dont be stugnant in idiology
 

mie najua Lisu ni intel. maana sifa kubwa ya intel ni ujasiri wa kusema ukweli mambo ambayo wengine wanayaogopa.ndimo akina Yesu, Yohana mbatizaji,Socrates, Jefferson, Martin Luther,Lumumba walimopita.kusema ukweli bila kupepesa macho. mimi mwalimu licha ya kutoka mkoa mmoja nakuthibitishia kuwa is the great human I have seen alive.kila likitajwa jina lake huwa machozi yananitoka kwa kumhusudu.Lakini ni vizuri kukiri na kusema udhaifu wake pia maana huko ndio kumpenda kweli.
By the way inaonekana historia ya Marekani huijui vizuri for your information anayependwa sana na kuenziwa sana ni Jefferson, Washington anashukuriwa zaidi kwa kumwendeleza Tom na kwa kuwa rais wa kwanza. jembe lao kubwa ni Tom likifuatiwa na mzee wa maamuzi magumu Lincoln

 
tundu:flypig::flypig: lisu nouma amewanyea patamu:rapture::rapture::israel::israel::rapture: hakuna kulemba mpaka kieleweke:flypig::flypig: m4c
 
He is an intelligent who has made an error
 

mi mbona maoni yangu kuhusu nyerere yalishabadilika muda hata kabla Tundu Lissu hajasema bungeni,kimsingi upande wa pili wa Mwalimu upo wazi katika vitabu na si katka historia inayofundishwa mashuleni,fuatilia hata Nasaha za Mihangwa.
 
Mtu asiye INTELLIGENT ni yule anayeabudu binadamu na viumbe wengine kama wewe unavyomuabudu Nyerere. Nyerere was a normal human being subjected to mistakes na kama ulivyo wewe alikuwa na vitu alivyoamini kuwa ni sahihi kwa mtazamo wake hata kama ilikuwa ni kinyume chake. Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake juu ya jambo lolote hata kama lipo kwenye biblia au msahafu. Iweje leo Nyerere au Karume wasikosolewe kwa mambo au makosa waliyofanya? Unadhani hao akina Abraham Linkohn hawana critics ndani ya Marekani? Mbona wao pamoja na Kennedy waliuawa kwa risasi na wamarekani wenzao.

Mtu aisye intelligent ni yule ambaye anaubaka uhuru wake mwenyewe kwa woga wa kutoongea ukweli kisa maslahi yake kisiasa au kiuchumi yatatetereka kama wewe unavyofikiria kwa TL. Kumbuka kuwa kizazi kinachomsujudia Nyerere ni hiki kinachoshika dola kwa sasa na wala si wale waliozaliwa mwaka 1980 ambao ndio wanaohitaji kushika dola kwa sasa.

Nyerere mwenyewe alisema UHURU wa KWELI ni ule wa jinsi kichwa chako kinavyofikiri. Kama katika umri ulionao bado akili na uhuru wako wa mawazo unatawaliwa na hisia za kuogopa athari zinazotokana na kusema kile unachoamini kuwa ni kweli basi bado unatawaliwa na ukoloni mbaya kuliko ule wa karne ya 19 na 20.

Kuna siku utashindwa kumwambia ukweli mkeo kwamba wewe umeathirika na VVU kwa kuogopa kuwa atakukimbia bila kujali madhara makubwa ya kutomwambia (Ni mfano tu).
 
Msamehe bure,unajua wakati mwingine wazazi hufanya maklsa ya kuwa watoto majina ambayo yana madhara,kama hili la TUNDU.
 
By Edwin Mtei

Nilisikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.

Edwin Mtei
Founder Chairman of CHADEMA
.
 
"Problem cannot be solved by the same level of thinking which created them".Albert Einsten
 
serikali wameuumbua kwa kusema uongo, walitegemea ingekuwa turufu ya kugomea majadiliano ya rasmu kama alivyofanya mnyika. Leo hawana la kuongea tena...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…