Bwana na Bibi Afya acheni kukaa maofisini piteni migahawani, wanachakaza afya zetu kwa tamaa ya faida kwasababu hawadhibitiwi wala kushitakiwa

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kuaharisha na kuugua matumbo limeshakuwa ni janga. Kulingana na mazingira ya kazi na umbali, inakuwa ni vigumu kurudi nyumbani ukale kisha uendelee na kazi.

Baadhi ya migahawa imekuwa ni janga kwetu wateja, mbinu hizi chafu hutumika kwa lengo la kukuza faida bila kujali afya zetu na huku ndipo matatizo ya cancer, miili kukosa nguvu, n.k huanza.

kununua nyanya mbovu zilizooza kwa bei rahisi ili kupata faida.

Kupikia mafuta machafu ili kuepuka kununua mafuta mapya kwa lengo la faida.

kutengeneza juisi na matunda mabovu ya bei rahisi ili kupata faida kubwa.

Uchafu, vyombo waosha ktk maji machafu

Kwenye nyama huko wala hakuelezeki wacha nikae kimya tu, ili kupunguza gahrama za nyama huwa kuna nyama aina flani zinauzwa kwa bei rahisi.
 
Suala la chakula ni jambo muhimu sana kuliwekea uangalizi, bila hivi hali itakuwa mbaya mno, naamini hata haya matatizo ya kukosa nguvu kwa asilimia kubwa ni kwajili ya migahawa kukosa uangalizi.
 
Kuaharisha na kuugua matumbo limeshakuwa ni janga. Kulingana na mazingira ya kazi na umbali, inakuwa ni vigumu kurudi nyumbani ukale kisha uendelee na kazi.

Baadhi ya migahawa imekuwa ni janga kwetu wateja, mbinu hizi chafu hutumika kwa lengo la kukuza faida bila kujali afya zetu na huku ndipo matatizo ya cancer, miili kukosa nguvu, n.k huanza.

kununua nyanya mbovu zilizooza kwa bei rahisi ili kupata faida.

Kupikia mafuta machafu ili kuepuka kununua mafuta mapya kwa lengo la faida.

kutengeneza juisi na matunda mabovu ya bei rahisi ili kupata faida kubwa.

mboga za majani za bei rahisi chafu ili kupata faida.

Kwenye nyama huko wala hakuelezeki wacha nikae kimya tu, ili kupunguza gahrama za nyama huwa kuna nyama aina flani zinauzwa kwa bei rahisi.
Kumbe Kuna nyama za Bei rahisi, ziko wapi tukanunue
 
Ulishawahi kuona muuza chips akimwaga chips za jana? Ni kwamba hazibaki au? Chukua na hilo
Mkuu kwan chakula kikibaki lazima tumwage? Mbona kuna namna nyingi ya kuhifadhi ili kisiharibike
 
Back
Top Bottom