Bwana yawezekana kupitia machozi haya kesho yangu haitakuwa hivi tena

Bwana yawezekana kupitia machozi haya kesho yangu haitakuwa hivi tena

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
BWANA YAWEZEKANA KUPITIA MACHOZI 😭 HAYA KESHO YANGU HAITAKUWA HIVI TENA

Mungu wangu nakushkuru kwa neema hii ya majira haya ya usiku. Ni mapenzi yako tu mimi kuendelea kuwa hai. Asante kwa neema hii🙏

Bwana yawezekana maisha ninayoishi leo au mapito ninayopitia nimesababishiwa na mtu au ni makosa yangu ya kibinadamu yamenifanya niwe katika majuto haya na upweke huu Bwana

Nashinda nikiwa mwenye huzuni nailazimisha furaha kwangu ila haidumu kwangu BWANA kwasababu sijapata amani ya moyo wangu

Hitaji la moyo wangu walijua vyema Mungu wangu, yatazame machozi haya na huzuni hii iliyotawala nafsi yangu, zitazame sadaka zangu na majitoleo yangu yakubalike mbele zako kwa ajili ya hitaji la moyo wangu nilitamanilo liwe

Naomba unitendee wema wako katika hitaji hili nilitamanilo, nina imani Mungu wangu utanijibu kwa furaha isiyo na kipimo na machozi yajayo yawe machozi yaliyobeba furaha na shukrani.
 

Attachments

  • 1731697757628.jpg
    1731697757628.jpg
    375.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom