Kumtishia Ethiopia halafu ukamuacha Uchina ambaye ndiye mjenzi na mfadhili wa bwawa hilo nadhani halijakaa sawa kabisa. Pili matumizi ya maji ya Nile siyo uamuzi baina ya Ethiopia, Misri na Sudan peke yao: Nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi ni wanahisa wakubwa ambao ni lazima washirikishwe kwenye hili suala. Mkataba wa Nile uliposainiwa hizi nchi zote kasoro Ethiopia zilikuwa chini ya ushawishi wa dola la Muingereza ndiyo maana sahihi zilikuwa za Waingereza na Wamisri tu.
Hili lisipoangaliwa linaweza kugeuka kutoka kuwa suala la kikanda tu (Regional Issue) na kufika kuwa suala la kidunia kwasababu litahusisha maslahi ya mataifa makubwa na hasimu ambayo yanagombania ushawishi barani Afrika, hasa kwenye ukanda wa pembe ya Afrika (The Horn of Africa). Misri ni mshirika mkubwa kimkakati (Strategic Partner) wa Marekani, usalama wake kisiasa ni ulinzi tosha kwa maslahi mapana ya Marekani hapa Afrika na Mashariki ya Kati.
Marekani hapendi jinsi Uchina anavyojisogeza kwenye ukanda wa pembe ya Afrika hadi kwenye nchi za Maghrib (The Maghreb), hivyo huu mgogoro siyo suala la maji peke yake: Kutengeneza ushawishi na nguvu vinahusika, maana kama bwawa hili likiisha, Ethiopia ndiyo litakuwa taifa mabalo linauza nishati ya umeme kwa nchi jirani kama Kenya, Sudan, Somali na Eritrea.
NB: Hata Tanzania ingeamua kujenga bandari ya Bagamoyo pamoja na Uchina ni lazima tungetafutiwa sababu kama ambavyo Ethiopia ametafutiwa sababu. Wafaransa husema C'est La Vie