Tusaidie tafsri, Mkuu.
===
Ila Egypt wana majivuno sana, wakati Eithiopia ni wastaarabu. Nilibahatika kuwa kundi moja na wote Wamisri na Waethiopia kwenye nchi mwenyeji huko! Aisee, wamisri walifikia hatua ya kuwadharau hata wenyeji wetu! Ikafika kipindi wenyeji wakawatolea uvivu hapo ndipo wakatulia. Walitaka kuleta ngebe niliwatoa nishai!
- - -
Ni rudi kwenye mada.
Mkuu ni kweli, kuisukasuka Ethiopia bila kujali nani wako nyuma yake ni kujidanganya. Na kwa sasa nimeelewa kwa nini China aliomba nafasi ya kuweka base ya kijeshi Djibouti.