Jidu, umekuwa kama jini lilolofungiwa ndani ya chupa. Wakati unayaeleza haya, bwawa liko kwenye hatihati ya kuvunjika kwa kuta zake na ikitokea hivyo huo ndiyo mwisho wake. Tunavyoongea wakazi wa Rufiji wapo kwenye hatari ya kusombwa na mafuriko yatokayo na ujenzi wa hili bwawa.
Kwa kifu bwawa lilijengwa bila kuangalia athari za kimazingira kutokana na jiografia ya eneo hilo. Hayo yote uliyoyaorodhesha yanaenda kusombwa na mafuriko badala ya kuwa neema tofuti na hizi theories zako. Kitu chochote kinachofanywa kwa kukurupuka siku zote mwisho wake ni mbaya.
Nafikiri wewe hat huo mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere hujafika.
Mimi nemefika na kujionea ujenzi.
Swala la kupasuka halipo, narudia halipo.
Bwawa limejengwa kwa ustadi mkubwa na wahandisi waliobobea.
Wengi hawajui kuwa sehemu ile yenye presha kubwa ya maji, kwenye msingi, bwawa lina ukuta mnene, sikosei, wa karibia mita 100( kiwanja cha mpira)
Pili, Kilichojiri ni maji kujaa katika muda mfupi kutokana na mvua zisizo za kawaida mwaka huu. Bwawa limejaa mapema kuliko muda uliokadiriwa.
Tatu , kwa nyie mliozaliwa majuzi, mafuriko ya mto Rufiji, hii si mara ya kwanza na imekuwa hivyo toka miaka ya 70 panapotokea mvua kubwa.
Nitakuwa mnafiki nikisema bwawa halijachangia, limechangia tena sana.
Bwawa la Mwalimu Nyerere lina urefu wa kilemeta 100, upana wa kilometa 25, na kina pale kwenye kinu cha kufulia umeme , kina cha mita 131.
Hayo ni maji mengi, na sasa hivi yapo na yana zidi kujaa kutokana na mvua za masika huko Mbeya, Ryvuma, Dodoma, Morogoro na kwingineko.
Tuanze kuondokana na fikra za kujifungia katika matatizo. Bado kuna fursa nyingi sana zinazotokana na bwawa hili na maji yake.