Bwawa la Nyumba ya Mungu na maisha ya wananchi

Bwawa la Nyumba ya Mungu na maisha ya wananchi

mwidaddy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2022
Posts
357
Reaction score
658
Sekta ya uvuvi imekuwa ni sekta pana inayoajiri asilimia kubwa ya Watanzania inayosaidia vijana kujiajiri na kutatua tatizo la upungufu wa ajira katika taifa letu kwa kiasi chake.

Taifa letu limejaaliwa rasilimali nzuri sana kwaajili ya kufanya uvuvi endelevu Tanzania kuna mito mikubwa kama mto Ruvu, mabwawa Mamkubwa kama bwawa la Mtera bwawa la Nyumba ya Mungu, kuna ziwa Nyasa, Tanganyika, Victoria, Eyasi, Manyara, pamoja na Bahari ya Hindi.

Licha ya resources zote hizo tulizojaaliwa bado baadhi ya mifumo katika usimamizi wa rasilimali hizo sio rafiki,

Na hapa nitazungumzia mifumo katika kulidhibiti bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo limeajiri vijana wengi kutokea mikoa jirani ya Kilimanjaro Arusha Manyara na Tanga.

Wasimamizi wa bwawa hili wanatumia nguvu kubwa isiyo rafiki katika maisha ya mtanzania hususan vijana, kuna kamata kamata nyingi uharibifu wa mali za wananchi ambazo wamezitafuta kwa fedha au mitaji ambayo wameipata kupitia loans, na wamepata loans kwa kuweka collaterals vitu vyao vya thamani kama nyumba, gari, viwanja ili wapate mitaji yao.

Askari kwa kushirikiana na Maafisa uvuvi wanachukua jukumu la kukamata wavuvi pamoja na wachuuzi na kuwapiga fines kubwa zinazowapelekea vijana na watu wengine waliojiajiri katika bwawa hili kufilisika mitaji yao na hata kushindwa kurejesha mikopo yao, na mwishowe kufilisiwa mali zao walizoziweka collateral kwa mashirika ya mikopo.

Kulifunga bwawa na kukamata watu sio njia rafiki ya kuidhibiti uvuvi haribifu katika bwawa hili, ni muda sasa wa kubuni njia mpya za kulilinda bwawa hili bila kuaffect maisha ya watu kiuchumi na kijamii.

kutoa elimu juu ya progressive fishing kwa kuinovate new strategies ambazo zitaendana na mabadiliko ya kimaisha pamoja na ongezeko la watu ambapo hazitoathiri maisha ya citizens na kulea mazao ya bwawa hili ni kitu muhimu sana.

Kiutaratibu pamoja na kazi za maafisa in any sector, is to easy the service na sio kuleta hardships, hapo Nyumba ya Mungu maafisa wamekosa ubunifu wa njia za kulidhibiti bwawa hilo mwishowe wanaishia kulazimika kutumia njia moja tu ya kufunga bwawa bila kuangalia wananchi wanaolizunguka hilo bwawa kama hawana ajira nyingine zaidi ya uvuvi, hali hii inatokana na uduni wa miundimbinu na maendeleo katika Maeneo hayo, na pia sasa wapo na makazi ya kudumu pamoja na familia zao ambapo ni ngumu kuziacha na kwenda sehemu nyingine kutafuta ajira kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, kuhama ilikuwa nirahisi pindi bwawa likifungwa kutokana na watu hawakuwa wengi na hapakuwa na permanent settlements kama ilivyo sasa.

Ni vyema jicho la karibu la mabadiliko na maendeleo katika bwawa hili litizame hilo, naamini wizara haishindwi kuleta maendeleo na wananchi wakafurahia kubarikiwa bwawa hili kwa kuendesha maisha yao ya leo na kulitunza bwawa hili kwaajili ya the future generations.
 
Back
Top Bottom