Kama mwananchi wa nchi hii na mlipa kodi nimesoma na kusikia kupitia magazeti, luninga na mitandao kuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere limejengwa chini ya kiwango. Naomba kuuliza maswali yafuatayo:-
(1) Kwanza Kampuni ya Misri iliyoshinda tenda ya ujenzi ilikuwa na uwezo, utaalaam, uwezo wa kifedha?. Kama sivyo kwa nini walimpa Mhe. Rais wa awamu ya tano OK kuwa Kampuni hii ina uwezo wa kulijenga bwawa hili. Inawezekana walimuogopa Mhe. Rais wa awamu ya tano kwa sababu ya kuogopa kutumbuliwa na wakamdanganya ili kazi iendelee.
(2) Je, ni Kampuni au ni Serikali iliyoteuliwa kutoa ushauri wa kitaalam?. Kama ni Kampuni binafsi inatakiwa iwajibishwe kwa kutosimamia ipasavyo taratibu zote za ujenzi kama ilivyo kwenye BOQ. lakini ni Serikali basi hii ni kosa kubwa sana kwa uamauzi uliofanywa na Serikali. Mwisho wa siku kutokana na hayo mapungufu Kampuni hiyo itakuja kuwaruka na kuitupia lawama zote Serikali.
(3) Nimesoma kuwa mpaka sasa ujenzi uko asilimia 44 tu ingawaje walitakiwa wakabidhi mradi June, 2022. Je sababu walizotoa zinaridhisha? Hapa najua watakuja na sababu ya Covi 19 na Matukio ambayo yako nje ya uwezo wao kama mvua n.k. Je Serikali imekaa nao chini na kupitia sababu zao kama ni sababu za msingi?.
(4) Kama kweli ujenzi uko chini ya kiwango ina maana dawa ni kuanza upya kwa maana kuwa yale mahandaki yanajengwa upya na kurekebisha kila kitu. Je, gharama ya marekebisho hayo nani atayabeba?. Hii ina maana kuwa muda wa kukamilisha ujenzi unaweza kwenda mpaka 2026.
(5) Je, kwanini Serikali imegeukia sasa suala la gesi na suala la Bwawa kama vile linapoapoa siyo kama zamani. Kwa hitimisho naishauri Serikali iunde Tume huru na waseme ukweli wa matatizo yote ya Bwawa hili ili taarifa ya Tume hii apelekewe Mhe. Rais ili aone la kufanya.