Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Nyie msiojua maana ya ujenzi mnasumbua jamvi.Kama mwananchi wa nchi hii na mlipa kodi nimesoma na kusikia kupitia magazeti, luninga na mitandao kuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere limejengwa chini ya kiwango. Naomba kuuliza maswali yafuatayo:-
(1) Kwanza Kampuni ya Misri iliyoshinda tenda ya ujenzi ilikuwa na uwezo, utaalaam, uwezo wa kifedha?. Kama sivyo kwa nini walimpa Mhe. Rais wa awamu ya tano OK kuwa Kampuni hii ina uwezo wa kulijenga bwawa hili. Inawezekana walimuogopa Mhe. Rais wa awamu ya tano kwa sababu ya kuogopa kutumbuliwa na wakamdanganya ili kazi iendelee.
(2) Je, ni Kampuni au ni Serikali iliyoteuliwa kutoa ushauri wa kitaalam?. Kama ni Kampuni binafsi inatakiwa iwajibishwe kwa kutosimamia ipasavyo taratibu zote za ujenzi kama ilivyo kwenye BOQ. lakini ni Serikali basi hii ni kosa kubwa sana kwa uamauzi uliofanywa na Serikali. Mwisho wa siku kutokana na hayo mapungufu Kampuni hiyo itakuja kuwaruka na kuitupia lawama zote Serikali.
(3) Nimesoma kuwa mpaka sasa ujenzi uko asilimia 44 tu ingawaje walitakiwa wakabidhi mradi June, 2022. Je sababu walizotoa zinaridhisha? Hapa najua watakuja na sababu ya Covi 19 na Matukio ambayo yako nje ya uwezo wao kama mvua n.k. Je Serikali imekaa nao chini na kupitia sababu zao kama ni sababu za msingi?.
(4) Kama kweli ujenzi uko chini ya kiwango ina maana dawa ni kuanza upya kwa maana kuwa yale mahandaki yanajengwa upya na kurekebisha kila kitu. Je, gharama ya marekebisho hayo nani atayabeba?. Hii ina maana kuwa muda wa kukamilisha ujenzi unaweza kwenda mpaka 2026.
(5) Je, kwanini Serikali imegeukia sasa suala la gesi na suala la Bwawa kama vile linapoapoa siyo kama zamani. Kwa hitimisho naishauri Serikali iunde Tume huru na waseme ukweli wa matatizo yote ya Bwawa hili ili taarifa ya Tume hii apelekewe Mhe. Rais ili aone la kufanya.
Nani kakuambia kuwa bwawa limejengwa chini ya kiwango. Na kiwango chenyewe kilichowekwa ni kipi?
Ujenzi wa bwawa si ujenzi wa nyumba yako ya kuishi, kuna kitu kinaitwa empirical construction, yaani unajenga kulingana na utafiti unaopatikana kadri unavyojenga.
Na hilo linahitajika kuwapo rock scientists na maabara zao, ambao wapo.
Sasa mtu unaposema mradi ukonyuma na umekamilika by 44%, ni bora ukaeleza matazamio yako.
Kimsingi mradi unaenda vizuri, na watnzania pale Stiglaz wana chakarika, tena ile mbaya.
Mradi wenyewe wa SGR sasa unaenda miaka mitano.
Watanzania tujue kuwa Three Gorges Dam limechukua miaka 10 toka 1994 hadi 2003, pamoja na uwezo wake mkubwa wa nchi ya China.
Rennaissance Dam la Ethiopia ilitazamiwa kuchukua miaka 9, 1911 hadi 2020, lakini hadi leo halija kamilika .
Haya masuala tuwe tunajua tunachokiandika.
Kujenga miradi mikubwa siyo sawa na kuagiza gari mtumba toka Japan.