Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato wametinga katika Soko la Kashai mjini Bukoba, usiku wa Julai na kushiriki kikao cha wafanyabiashara wa soko hilo.
Wafanyabiashara wa soko hilo walikutana jana Julai 15, 2024 usiku kwa ajili kushiriki kikao kilichokuwa kikijadili namna ya kuboresha soko hilo ambalo linatakiwa kufanyiwa maboresho lililopo mjini Bukoba mkoani Kagera.
Mawaziri hao walifika sokoni hapo mida ya saa 2 usiku na kupata fursa ya kuzungumza nao kisha wakawapongeza wafanyabiashara hao kushiriki kikao hicho ambacho nao walikuwa wakitoa maoni yao ya kuboresha soko hilo baada ya kuona michoro ya awali kisha na wao kueleza nini kifanyiwe maboresho.
Waziri Nape ambaye alifika mkoani humo kwa ajili ya kuendelea na ziara yake mikoa ya Kanda ya Ziwa ya kukaguwa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano inayojengwa mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo anatembelea mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga.