BYD Shark 6: Wabongo hawataki Masihara, Mil 170+ kabla ya TRA sio poa!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Walivyofungua dealership ya kuuza 0 km kuna watu wakajua watafeli. Ila naona vyuma vinatoka.

Hii Shark 6 inakuja kupambana na kina Navara, Hilux au Ranger. Ila yenyewe ni PHEV, ina engine ya cc 1500 au 2000 kwa performance, zote turbo i4.

Kwa umeme peke yake unaweza kwenda km 85 ila kwa vyote unavuka 700 km.


Ni chuma ya kishua sema bei imesimama, hapa mchawi TRA maana kwenye kikokotoo siioni.
 
Gari za umeme kwenye kodi ni ndogo sana ,haitishi bro
 
Mkuu hadi kodi hadi barabarani itakuwa ngapi?
 
Mwezi uliopita nilipishana nayo moja ya rangi nyeusi pale kariakoo kamata .
Chuma zina muonekano wa pekee kila MTU alikuwa anaishangaa
Duh anapata wapi moyo wa kwenda nayo Kariakoo. Muuza miwa kwenye mkokoteni akichubua.
 

Hawa BYD, Jetour n.k waanzishe utaratibu wa kununua chuma kwa monthly plan kama ilivyo China, USA, Europe n.k

Wasio na uwezo wa kunua kwa cash wawe nao na namna ya kumiliki chuma kalk
 
Kikokotoo cha TRA ni kwa gari zilizokwisha kutumika au kua na usajili nje ya Tanzania,
Gari ambayo haina usajili kama,
Toka kutengenezwa unalipia
18% kutoka kwenye pesa ya manunuzi
Railway Levy fee
Port Charges na zingine chache nilizosahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…