BYD wazindua magari yao maarufu matatu ya umeme (Dolphin, Seal na Atto 3) nchini Kenya

BYD wazindua magari yao maarufu matatu ya umeme (Dolphin, Seal na Atto 3) nchini Kenya

Sisi ndio kwanza tunaporutubisha mahusiano na wazalishaji na wamiliki wa visima vya mafuta. Ndio kwanza tunajenga vituo vya mafuta mpaka mitaa ya makazi. Maendeleo ya EV ni ndoto. Kuna vijana wa DIT waliwahi kuunda gari ya umeme japo finishing yake haikuwa ya kuvutia, ilikuwa inaletwa kwenye maonyesho, kila mwaka na mawaziri wanakuja wanaikagua inarudi Dar kwa miaka 2 mfululizo. Serikali ingewapa mtaji vijana hao na kuwaongezea watalaam leo tungekuwa mbali. Kenya wametumia technology ya nje. Uganda wametumia zaidi vijana wa ndani. Tanzania hatuna hata wazo zaidi ya kupandishiana bei ya mafuta.
Tutaachwa na kila teknolojia. Tutakuja shtuka tumechelewa.
 
Aisee Kwa style hii Acha tuchange pesa Tu, haya magari kila MTU anatamani KUMILIKI
Kuchajia home cheap kinoma ila slow. Ukirudi home unachomeka charge unaenda kulala. Unakuta hadi asubhi imetoka 30% hadi 70% hivi.

Hiyo unakuta hadi range ya kilometa 300 sasa kwa misele ya kawaida mzee si siku 4 izo.
 
Safi sana...Maana yake sasa itakuwa rahisi kuendesha magari, maana unachaji t hahuhitaji petroli. Sisi hatuwezi kwenda huko, sababu , bado tumemkumbatia mwarabu. Na tunahangaika na gesi...Ila gari za kuchaji ndio zenyewe.
Yakiwa mengi, kodi zilizo kwenye mafuta zinahamia kwenye umeme, shida inakua ni ile ile
 
Bado iko juu, hata tukigundua mafuta yetu yatauzwa kwa bei hizo hizo za juu.
Nakumbuka, wafadhili wa mradi fulani hapa Tanzania ,siwezi kuutaja toka Scandinavian countries, wao kwao, ulaya wanaenda ofisini na baiskeli ili ku save hela kutusaidia. Walipokuja kukagua mirafi hapa kwetu, wakashangaa fedha hazijapelekwa kwenye mradi walivyokusudia, badala yake wamenunua land cruiser vx kuendea kuangalia miradi. Sasa linganisha mfadhili anatembelea baiskeli ya laki 2, maskini anayefadhiliwa ananunua vx ya milioni 600.
 
Si tumekalia uchawa na ccm tu
Atleast kwenye ili wangejatibu kua serious.

Ila kuna kitu labda kinachezwa na hawa madon wanaoimport mafuta au wenye vituo vya mafuta.

Kuna mtu katolea mfano wa internet service ya Elon Musk, StarLink.

Imewekewa vikwanzo hadi haijaja, tunaamini hii mitandao ya simu inahusika kwasababu inajua kwenye internet ndio wanakotupata.

Possibly same inatokea kwenye hawa jamaa wa mafuta.
 
Watanzania tupo matakoni mwa dunia.

Kama taifa hatujui tukitakacho, sera zetu mbovu mwaka wa 60+ toka tupate uhuru, sisi ni kujenga mashimo ya choo, maji mtihano, umeme shida, huduma za afya kero, barabara..
Viongozi wetu mafisadi waliokubuhu.
Wanafisadi halafu hawafanywi kitu chochote refer report ya CAG
Wangekuwa wanashikishwa adabu huu upumbavu usingekuwepo
Hawa wahuni wangeona mali ya umma kama hatariiii sio ya kuchezea
 
Tatizo la Tanzania ni uongozi na pia elimu yetu ni finyu. Hivi umeshawahi kuangalia bunge la Kenya ukaona majadiliano yao? Wabunge wanaongea mambo ya maana na wanajua kiingereza. Unaona kabisa ni watu wenye upeo na elimu yao inawasaidia. Sisi huku kwetu kina Kibajaji na Kasheku wanaweza nini? Bunge zima limejaa mapambio ya kumsifu Samia. Hata level ya urais huwezi kumlinganisha Ruto na Samia. Kwa upeo alionao, Samia hawezi kupata ubunge Kenya.
Bongo ni uchawa tu, vyeo wanapeana kwa ahsante na kujuana.
 
Back
Top Bottom