Bye bye ios

Bye bye ios

Baada ya miaka kama 7 hivi kuwa mtumiaji mzuri wa ios phone (iPhone) hatimae huu mwaka nahitaji kujiondoa rasmi.

Sababu ya kujiondoa ni kutokana na kupangiwa baadhi ya mambo ikiwemo kunyimwa Uhuru kwenye chombo changu.

Maana siwezi kudownload Movie, Siwezi kudownload Nyimbo mbalimbali yaani wao ni mwendo wa Kula Bando Tu kila sehemu sasa nimeamua kujitoa rasmi.

Sasa Nimeamua kurudi kwenye Android zetu hizi zenye Uhuru wa kuifanya unavyotaka ila nimeshindwa kuchagua ni simu gani nzuri kuanzia utunzaji wa chaji, ubora wa Camera, na Speed ya internet kama 4G.

Nimejaribu kutembelea madukani nimekutana na Samsung nyingi lakini katika process ya kucheki specific zake nakutana na chip za MTK tu, nimeshindwa kuelewa inamaana siku hizi Samsung wameamua kuhamisha simu zao kutoka Qualcom Hadi kwenda Mtk. Na Mimi chip ya Mtk huwa siziamini kabsa.

Wadau naomba maoni yenu ni simu gani nzuri hapo

Oppo, Samsung, Nokia, Redmi.


Bajeti yangu ni Laki Tano.
Samahani kidogo mkuu kwa bajeti ya laki tano ilikuwa unatumia iphone ipi?
 
Redmi note 10 ni around laki 4, unaweza ongeza kidogo uka chukua version ya 128GB, ina kioo cha Amoled itakusaidia suala zima la kuangalia movies.

Ahsante mkuu shida huku kwetu Redmi bei zimechangamka sana.
 
Redmi note 10 ni around laki 4, unaweza ongeza kidogo uka chukua version ya 128GB, ina kioo cha Amoled itakusaidia suala zima la kuangalia movies.
Mkuu hivi muvies nzur tunazipakulia site ipi, napenda muvi ila playstore kuwatch online ndio kazi matangazo kibao na sipati movies nzuri
 
#FAHAMU MFUMO wa Android kwa sasa unatumika na zaidi ya Vifaa Bilioni 3 duniani, hii inajumuisha simu, saa, magari, TV, tablets na vifaa vyote vinavyotumia mfumo huo.

#NipasheMwangaWaJamii #NipasheHabari
#NipasheTehama https://t.co/oiYsOaeaFZ
 
Mkuu Ahsante Kwa kumfafanulia


Sasa najiuliza nimecheki hapa Samsung A32 5G ina chip ya Mtk na ukiangalia Mtk nyingi kama Tecno zinavyozinguaga baada ya wiki Tu zinaanza kustack na kupostop app Nimeamua Nikimbilie humu nipate aghalau mwanga.
Hiyo tecno itakua ya huko bumbuli kwenu

Japo situmii tecno lkn huo ni uongo
 
Back
Top Bottom