I see some bragging hapa ikichukua mkondo.....lol.... Message itafika kwa mama Matesha.
Katika Ulezi mara nyingi akina mama tupo strict saana kwa watoto hasa wa kike. Baba nae anaweza kua strict lakini sio kwa level za mama. Mimi kama mama - na hasa tokana na makuzi kua mtoto wa kike lazima a master kila kitu nyumbani.... Inakufanya utake the same for your kid. Utahakikisha wakapangia responsibilities tokana na level ya Ukubwa wake, toka kupika chai hadi kupika ugali, toka kusuza kikombe hadi kuosha vyombo, toka kufuta maji yalo mwagika to the level ya kupiga deki. Mara nyingi (for hata mimi ilikua hvio) unaona kama mama ni mnoko fulani, hakupendi, anapenda tu kukutumikisha na the like....
Baba yeye akiwa na mtoto wa kike anchowaza cha kwanza ni jinsi gani amtimizie binti yake asifanyiwe na ma bazazi yale yeye baba afanyavyo kwa watoto wa wenzie, ama dada wa wenzie na wanawake woote. Wanaume wengi wanaamini kua toka utoto akidhibiti penzi la mtoto wake wa kike na kumtimizia kila kitu mwanae walau ataepuka kikombe cha kurubuniwa huko mtaaani (Yes it helps to some extent) but ukweli unabaki pale pale no matter how she Loves you... She will eventually fall in love.... Kwa muktadha huo yeye binti huona kua baba is the best parent, lolote atakalo apewa, anadekezwa na baba anamjali na kumuulizia kila saa.... Tena sa ingine hata hua amwambia mama kua ampunguzie kazi.....
Na nature tu, wa kiume kwa mama wa kike kwa baba.... Mtoto wangu wa kiume.... ni mdogo, ana wivu huyo hataki kabisa mtu mwingine apate attention yangu hasa kama ni opposite sex.... anakua mkali kabisa na tu amri twa hapa na pale....