"Bye Daddy"...... Dah!!!

"Bye Daddy"...... Dah!!!

Wajameni salaam kwa mpigo.

Ukubwa dawa wajameni......

Hii biashara ya mabinti na baba zao kuwa "washkaji" sijui imetokea wapi. Jana nlikapeleka kabinti kangu kapendwa shule kuanza maisha rasmi ya boarding. Shule imekomaa mabinti lazima wahamie hostel kwa ajili ya maandalizi ya "kufa mtu" ya mitihani ya kitaifa mwaka huu. Ikawa haina jinsi.....Sikuwahi kuwaza kabinti kangu kataenda boarding katika elimu ya msingi asee.....

Tumekapeleka haka kabinti nikiwa na mama yake.... wakati ndo tunamkabidhi kwa "wazazi wake wapya" kabinti kakatoka mbio na kunirukia na kuniambia "Bye daddy"... kisha hakooo kakatokomea..... Cha kustaajabisha, mamake alipewa bye ya mbaaaali lol

Hii "bye daddy" bado haijatoka masikioni asee.... kwamba ntarudi home leo bila kulakiwa na kamatesha kangu... damn!.... Na haya maisha ya mimi na mama Matesha wangu kubaki peke yetu nyumba nzima, si honeymoon nyingine hii wajameni? Atanikomaje?

Baada ya kusema hayo naomba msaada...... Eti kuna kitu gani kinawafanya mabinti "wazimike" namna hii kwa baba zao? Ni kwanini mababa wengi nao pia wanakuwa kama "wamelogwa" na mabinti zao? (Hapa ODM nakiri, vibinti vyangu navizimikia kinoma asee... tena haka kamatesha ndo usiseme.....)

Bye Daddy... dah!


Ha ha ha hahaa hommie mi nimeona hapo kwenye nyekundu tu..
 
I see some bragging hapa ikichukua mkondo.....lol.... Message itafika kwa mama Matesha.


Katika Ulezi mara nyingi akina mama tupo strict saana kwa watoto hasa wa kike. Baba nae anaweza kua strict lakini sio kwa level za mama. Mimi kama mama - na hasa tokana na makuzi kua mtoto wa kike lazima a master kila kitu nyumbani.... Inakufanya utake the same for your kid. Utahakikisha wakapangia responsibilities tokana na level ya Ukubwa wake, toka kupika chai hadi kupika ugali, toka kusuza kikombe hadi kuosha vyombo, toka kufuta maji yalo mwagika to the level ya kupiga deki. Mara nyingi (for hata mimi ilikua hvio) unaona kama mama ni mnoko fulani, hakupendi, anapenda tu kukutumikisha na the like....

Baba yeye akiwa na mtoto wa kike anchowaza cha kwanza ni jinsi gani amtimizie binti yake asifanyiwe na ma bazazi yale yeye baba afanyavyo kwa watoto wa wenzie, ama dada wa wenzie na wanawake woote. Wanaume wengi wanaamini kua toka utoto akidhibiti penzi la mtoto wake wa kike na kumtimizia kila kitu mwanae walau ataepuka kikombe cha kurubuniwa huko mtaaani (Yes it helps to some extent) but ukweli unabaki pale pale no matter how she Loves you... She will eventually fall in love.... Kwa muktadha huo yeye binti huona kua baba is the best parent, lolote atakalo apewa, anadekezwa na baba anamjali na kumuulizia kila saa.... Tena sa ingine hata hua amwambia mama kua ampunguzie kazi.....

Na nature tu, wa kiume kwa mama wa kike kwa baba.... Mtoto wangu wa kiume.... ni mdogo, ana wivu huyo hataki kabisa mtu mwingine apate attention yangu hasa kama ni opposite sex.... anakua mkali kabisa na tu amri twa hapa na pale....

U nailed it!
 
Na Ma matesha, honey moon
ya jubilei ya miaka mingapi vile?
Mpaka akomeshwe tena.
Byee Dadyyy
 
Yeye mbona mkorofi? Kwanza nina hasira nae....
hahaaa, ugomvi wenu na babu me siuwezi.

Jamani Madabwada ako busy, but he is good na salamu zimefika.....
nashukuru kama salamu zimeshafika punde hii ... kwa kumuenzi babu "with this wonderful thread", naomba pia leo umsikilizishe mzee ile kitu mpya ya jahazi 'my chocolate'.
 
Babu mbona unanichunia kama hujaniona leo? tuna ugomvi?
Nimekuchuniaje mpenzi? Niko hapa nawasomeni huku namtumikia mkoloni. Nikuchunie tena? Afu niinjoi na nani?
 
lol, inabidi ujipange mamie, kama ni mzee wa kiti kirefu kama babu yetu then wenyewe wanasema lazima ataanza binti tu!
Khaaaaaa!
Mbona hii theory siifahamu!!!!
Ayaaaaa,kwisha habari yangu lol!
Itabidi nijiandee tu km hiyo formula ni valid lol!
 
nna kabiti kakike ka darasa la tano, mama ake akimuamsha asubuhi hataki mpaka dady niende kumuamsha, asubuhi kabla hajaenda shule anywi chai mpaka niwe nae mezani, nikichelewa kurudi nyumbani usiku mama atakoma, ataiba simu ya mama yake anipigie aulize niko wapi. she is the only kid at home at the moment.
 
Back
Top Bottom