CAF Champions League: Al Ahly vs Yanga 20/04/16

CAF Champions League: Al Ahly vs Yanga 20/04/16

Kwa mara ya kwanza nilikuwa naishabikia yanga bila kujijua, uzalendo ni shida!
Yanga wazembe sana, walianza kujilinda mno kusubiri matuta.
Wamejitahidi ila wameniudhi, waarab walikuwa wanafungika hawa! Tungetoa gundu maana ktk matuta kina kitu kiliniambia yanga angepita. Tooo bad, sekunde ya mwisho?? Dah!

Jamaa wametukimbiza sana, mwanzo hadi mwisho, nadhani tuliishiwa pumzi. Siyo mbaya, hatua tuliyofikia imewaduwaza hata wao.
 
Game over...

Yanga tumejitahidi though

Dakika ya 96 Alhy wanapata goli la 2
Kumbe siku hizi mpira siyo dakika 90 tena? Hivi jamani mpaka dakika hizo Yanga tumeshindwa kupaki basi twende kwenye matuta? Mimi ndio maana sitaki kuwa mshabiki sana wa hii mipira inauma sana na afadhali sijaangalia mechi yenyewe.
 
Hivi jamani huyu jerry muro ataacha lini kuropoka?huyu ndo anayesababisha hadi timu kufungwa.
 
Da!mimi Simba ila nilikuwa nataka Yanga ishinde ila bado wachezaji wetu bado wana kushangaa uwanjani maana beki alikuwa na uwezo wa kuokoa ila akasubiri mpira umfikie mguuni.
 
Wakichangani walitutabiria goli 4 au 5 furahieni nashangaa ya kwenu yamewashinda hata kibonde anaeshuka daraja coastal inawatoa jasho ?na kuwatoa kwenye mashindano bora yanga anaetolewa na timu za kimataifa kuliko nyie muwe na uzalendo jamani hata kidogo.
 
Hasira haziui la sivyo sa hv ningekuwa na jina jingine yaani nyota imezima ghafla, nitamwambia nini huyu jamaa angu wa matopeni???????????????????????????
 
Washabiki wa Simba waliokuwa wanaishangilia Al Ahly ndo wamesababisha Yanga kufungwa goli la pili.
 
Haya hamieni La liga Barcelona anaua leo.

Dakika ya 81 mtu Kala 8-0.
 
Wakichangani walitutabiria goli 4 au 5 furahieni nashangaa ya kwenu yamewashinda hata kibonde anaeshuka daraja coastal inawatoa jasho ?na kuwatoa kwenye mashindano bora yanga anaetolewa na timu za kimataifa kuliko nyie muwe na uzalendo jamani hata kidogo.
Maneno ya mkosaji haya.teh teh teh...
 
Back
Top Bottom