CAF Champions League: Al Ahly vs Yanga 20/04/16

Hongereni wamadimbwini.Karibuni mchangani.Jina la wakimataifa life rasmi kuamzia leo.
 
Japo mie sio mshabiki wa Yanga, nawapa hongera kwa kucheza vizuri. Mpira ulikuwa na ushindani. Sio kama ule wa jana wa timu yangu ya Azam.
 
hongera ya Yanga kwa kujaribu msubiri mwaka ujao labda atasimama upande wao
 
Jamaa wametukimbiza sana, mwanzo hadi mwisho, nadhani tuliishiwa pumzi. Siyo mbaya, hatua tuliyofikia imewaduwaza hata wao.
Ila walikuwa wanafungika hawa waarab, ishu ni yanga walianza kupaki basi, ila kwa kweli wamejitahidi sana.
 
Nimeangalia kupitia ch. ya kiarfabu
basi ni heluuua heeeluaaa heeeeluuuuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa sijui ndo goooooooooooooooooooooooooooo
 
Ilikuwa ni poor marking kwenye krosi ya shambulizi...Hata goli lao la kwanza ni poor marking ya kona
Mimi bado hainiingii kabisa akilini timu inacheza ugenini dakika zimeisha mnashindwa kupaki basi na mnaruhusu goli, kwakweli mimi ushabiki wa mpira siuwezi haya mambo yanaudhi. Penati huwa hazina mwenyewe tumepoteza nafasi adimu ya kuandika historia mpya leo.
 
Jamani kifo ni kifo tu, iwe kwa ajali au kuumwa ni kifo tu.
cc : Jerry Muro
 
Timu zetu zijifunze kucheza mechi mbalimbali za kirafiki na hizi team kubwa Africa lasivyo tatizo la uzoefu litasumbua daima
 
nafikir ligi yetu inachangia huwezi ukawa unashinda kila mechi kirahisi hlf ukategemea kushinda kwenye mpira wa kasi kama ule. hata hivyo yanga wamecheza mpira wa nje ya bongo league
 
Hatujatoka bali tumeshuka ngazi moja chini tunaingia mtoano mwingine ila cha ajabu utashangaa tena YANGA vsMAZEMBE
 
Da!mimi Simba ila nilikuwa nataka Yanga ishinde ila bado wachezaji wetu bado wana kushangaa uwanjani maana beki alikuwa na uwezo wa kuokoa ila akasubiri mpira umfikie mguuni.
Kwa kweli hata mimi ni simba ila leo nilikuwa na yanga kwa dhati kabisa, nimejikuta tu nawashabikia. Nimeudhika sana kufungwa goli dk ile.
 
hii imetupeleka kwenye upande wa tp mazembe.lakn naona yanga mwaka huu tutafka robo fainal ya kombe la shirikisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…