John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inaendelea kwa sasa, ni msimu wa 2021/22 lakini kuna matukio kadhaa ambayo inawezekana yakawa na maana tofauti kuhusu soka la Afrika.
Wababe wa Misri, Al Ahly licha ya kuchukua nafasi ya tatu hivi karibuni katika Klabu Bingwa Dunia walipoenda kushiriki, lakini wamejikuta wakipoteza mchezo wao tena kwenye uwanja wa nyumbani katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kitu ambacho ni nadra kutokea.
Al Ahly wamepigwa bao 1-0 na Mamelodi ya Afrika Kusini, jana Jumamosi Februari 26, 2022 katika mchezo wa Kundi A.
Kabla ya hapo Mamelodi Sundowns ilikuwa ikiambulia sare tu tena ikiwa kwao Afrika Kusini, lakini sasa hivi wameichapa Al Ahly tena wakiwa Misri.
Kumbuka kuwa Al Ahly pia katika mchezo wa kwanza wa hatua hiyo waliambulia matokeo ya 0-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambayo ndiyo inayoshika mkia.
Upande mwingine, wababe wengine wa Misri, Zamalek wapo kwenye hali mbaya katika michuano hiyo, wakishika nafasi ya tatu kati ya timu nne katika Kundi D.
Zamalek hawajashinda katika mechi tatu, wana sare mbili na kupoteza moja, nao pia jana waliambulia kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Wydad AC ya Morocco.
HII MDAU UNAONAJE, NI ANGUKO LA WAKUBWA WA MISRI AU NI UPEPO TU MCHAFU WATAREJEA KATIKA MSTARI AU SOKA LA NCHI NYINGINE LIMEKUA?