kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Yanga imeamuliwa na caf kulipa TZS 82,0000 kwa kosa la kuvunjwa vioo vya gari lililotumiwa na RIvers United ya Nigeria hapa tanzania, rivers kuibiwa fedha kwenye basi, mashabiki wa Yanga kumulika vitochi (laser) na kuwasha moshi uwanjani. Hukumu kama hii ina harufu ya ushabiki wa simba na Yanga huko caf.
Tuliona vitochi uwanjani kwenye mechi zote zilizochezwa usiku kwenye mechi zote, waarabu wanawasha moshi unaotoa rangi za timu zao, Simba waliwamulika wapinzani wao siko kwa vitochi tu bali yuko jamaa aliwamulika na lijitochi la kuwindia lakini hakuna faini hizo. Rivers united wanasafirije na mamilioni ya fedha kwenye basi kubwa kama lile na je, nani alithibitisha wizi huo wakati wizi ni kosa la jinai linalohitaji uchunguzi na hukumu za kimahakama? Ni nani kwamaana mkemia yupi alidhibitisha kuwa gari la rivers lilipuliziwa sumu?
Hukumu ya kipuuzi kama hiyo imetolewa sasa ili kuitoa Yanga mchezoni wakati huu wanajiandaa na mechi yake na marumo, Hii haina tofauti na ile ya Fei toto kuleta fujo siku moja kabla ya mechi na Azam. Huu ni mtego wa kipuuzi ambao una lengo ya kupunguza vibe na maandalizi ya mechi hiyo ya nusu finali.
Wanashindwa kuizuia yanga uwanjani badala yake wanajaribu nje ya uwanja. Hakuna kesi hapo ni porojo tu za mtaani zinazotokana na shinikizo la utani wa jadi uliojipenyeza huko caf. CAF inajishushia hadhi kwa kuwa na watu kama hawa kwenye management ya kutoa maamuzi.