CAF kupitia barua yao imewaambia TFF na Simba SC kuwa mchezo wa fainali ya pili ya CAFCC kati ya Simba dhidi ya Berkane ipigwe New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Taarifa za uzushi hizi, CAF siku zote wakiona kiwanja ulichochagua hakina vigezo wanakuambia uchague kiwanja kingine ili kucheza mechi yako. Iweje leo iwe tofauti na kuamuru mechi ichezwe sehemu fulani. Mm nakataa kabisa na nitakuwa mtu wa mwisho kuamini hili.
Madhara ya kuleta uchawa kwenye mambo ya msingi ndio haya.
Binafsi baada ya Simba kutinga fainali nikauliza fainali ya CAF ni jambo kubwa ni mojawapo ya vitu tunavyoweza kuvitumia kujitangaza kama nchi nikauliza mechi itachezwa wapi na uwanja wenyewe wa mkapa ndio kama vile tulivyoona ukigeuka kuwa shamba la mpunga? Nikajibiwa na Naibu waziri Mwana FA kuwa mkapa unakarabatiwa eti mkandarasi mbobevu kaajiriwa kufunga mabomba yanayotoa maji uwanjani nikajisemea muda utaongea
Mamia Samia alitumia mabilion kutengeneza royal tour Ili kuitangaza nchi Ina maana hii issue ya Simba kuingia fainali hawakuona kama ni mojawapo ya vitu vinavyoweza kuitangaza nchi?