CAF yaamuru mechi ya fainali Simba Vs Berkane ichezwe New Amaan, Zanzibar Mei 25, 2025

CAF yaamuru mechi ya fainali Simba Vs Berkane ichezwe New Amaan, Zanzibar Mei 25, 2025

Hapo basi bingwa ni berkane

Ila serikali hii wametisha,pesa imetolewa 2023
Tuna kiwanja kimoja ni vipi siku tukiwa na viwanja vitano?,tutaweza kukarabati kweli
 
Wakuu!

CAF kupitia barua yao imewaambia TFF na Simba SC kuwa mchezo wa fainali ya pili ya CAFCC kati ya Simba dhidi ya Berkane ipigwe New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

CAF imesema uamuzi huo ni baada ya kujiridhisha na ukaguzi wa uwanja wa Benjamin Mkapa katika vipindi vya mvua.

Hata tukicheza kwenye bwawa la kambale bodo tutawafunga tu.

Hatoki mtu weweeeee!
 
Simba hatupeleki timu, huko Zanzibar tutaingiza vipi mbuzi?
Dah! Watu walishafukia mbuzi wao kitambo! Inakuwaje wakafukuliwe na kuhamishiwa Zanzibar? Na muda wenyewe wa kufanya hivyo hata hautoshi!

Hapa dawa pekee iliyobaki ni kususia tu kucheza hiyo mechi yao. Sisi simba hatutaki kabisa kuonewa na mtu.
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini hizi taarifa mpaka nione source inayoeleweka
Ndio imeshakua hivyo, labda cha kushauri madumu ya mafuta ya upako na viloba vya chumvi vinavyo tumiwa na Simba kupata ushindi, Haraka vianze kupelekwa Aman Stadium kwa matumizi ya mechi ya marudiano
 
Simba wakatae kabisa hili.Mechi ipigwe kwa mkapa please please
 
Taarifa za uzushi hizi, CAF siku zote wakiona kiwanja ulichochagua hakina vigezo wanakuambia uchague kiwanja kingine ili kucheza mechi yako. Iweje leo iwe tofauti na kuamuru mechi ichezwe sehemu fulani. Mm nakataa kabisa na nitakuwa mtu wa mwisho kuamini hili.
Na ndivyo ilivyo, hili la kulazimisha kucheza sehemu fulani, sio CAF labda wengine wamehusika kushinikiza. Lol
 
Khaaaa basi sawaa tusubiri tuone kwanza huko kwao nn kitajiriii
 
Caf washikirie hapo hapo tuko nao bega kwa bega
Motsepee babaaa sepa na kolopwinyoo
Hapa berkane lazima wapige kama chapati
 
Kama ni kweli bc safi sana, viongozi wa TZ ni wazembe wamebaki na jitihada za upigaji mana sio mara moja wanatuambia uwanja umekamilika
 
Wakuu!

CAF kupitia barua yao imewaambia TFF na Simba SC kuwa mchezo wa fainali ya pili ya CAFCC kati ya Simba dhidi ya Berkane ipigwe New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

CAF imesema uamuzi huo ni baada ya kujiridhisha na ukaguzi wa uwanja wa Benjamin Mkapa katika vipindi vya mvua.

Sasa itakuwaje wakati tushaandaa mbuzi na waganga wetu pale,,Ina maana berkane na wao wametufanyia ubaya ubwela sijui nani kawapa za ndani kwamba pale kwa mkapa uwa tunafanya mambo yetu na tukicheza kwingine mambo yanakuwa magumu🤣🤣🤣
 
Uchawi mbaya sana ...
Simba na ifutwe kabisaa ..
 
Back
Top Bottom