CAF yafungia uwanja wa Mkapa

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,043
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limefungia Uwanja wa Benjamini Mkapa kutotumika kwa kile kilichoelezwa umeharibika eneo la kuchezea (pitch) na sasa utafungwa kwa mwezi mmoja kupisha marekebisho.

Source: Mwanaspoti
Uzembe wa wasimamizi wa uwanja.
 
Heeeeeeeeee! sasa wale wa hatoki mtu kwa Mkapa je?
 
Yaani mpaka mamlaka za juu zaidi ziamue? TFF wameshona vitambi tu na kufurahia blahblah za simba na yanga na feitoto. mamlaka za usimamizi za uwanja zipo na kuja na blah blah za kuwa nyasi zimeshambuliwa na fungus

Tunashuhudia viwanja vya wenzetu huko vinakuwa sagi na vya kuvutia licha ya kutumika sana
 
Hivi vyoo vya huo uwanja vilirekebishwa?
 
Uwanja wa Benjamin Mkapa (Lupaso) haujafungiwa na CAF kama inavyosambazwa na watu mtandaoni.

CAF walituma wakaguzi wao ili kukagua uwanja na miundombinu mingine itakayotumika kwenye shindano la Super Cup ya Afrika.

Wakaguzi walifika hatua wakakaa na wamiliki ambao ni Serikali na wakawaeleza vya kurekebisha na Serikali ikaomba hiyo ripoti itumike kwenye marekebisho kwakuwa Benjamin Mkapa ni moja ya viwanja 7 ambavyo viko kwenye mpango wa marekebisho chini ya Serikali.

Taarifa nilizonazo kwenye ukaguzi ni kwamba wakaguzi walisema sehemu ya kuchezea ina 3% tu nje ya 100. Walisema eneo hilo ni bovu na kwa shindano lao ambalo ni la kiwango cha FIFA.

Dressing rooms pia walitolea maoni kwamba ni eneo linatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa. Technical areas pia wanasema ni ya kizamani hayatakiwi kuwepo. Mambo mengi yameanishwa ila hakijafungiwa.

Maliwatoni nako walikutolea kasoro na kusema tuna majengo ya kiwanja lakini uwanja wa mpira haupo.

Serikali wamepewa hadi mwezi Mei kufanya marekebisho na watakuja kukagua tena kabla ya mashindano ya Super Cup kuanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…