Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Klabu ya Simba Sports Club imekumbana na adhabu mpya kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) huku ikijiandaa kucheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United Jumapili, Septemba 28, 2025, bila mashabiki na faini ya Dola 50,000 (takriban Sh123 milioni).
Adhabu hii ni kuongezwa kwa faini ya Dola 30,000 (Sh74 milioni) iliyoletwa kutokana na makosa yaliyotendeka kwenye mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane Mei 25 mwaka huu.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amethibitisha adhabu hizo na kuwaasa mashabiki kuwa makini ili kuepuka kuigharimu klabu. Ally alisema, "Hasara ya kwanza tunakosa mashabiki, hasara ya pili tunakosa mapato na hasara ya tatu tunalipa faini. Vilevile tumepewa adhabu kutokana na mechi ya fainali dhidi ya RS Berkane, huku vilevile tuliwasha fireworks. Jumla tumetozwa Dola 85,000 sawa na Sh200 milioni."
Aidha, Ahmed Ally amesema kuwa klabu itaendesha zoezi la mchango kwa mashabiki kupunguza mzigo wa deni hilo na kusisitiza umuhimu wa kuboresha taswira ya ushabiki. "Tunacheza bila mashabiki kwenye mechi dhidi ya Gaborone United pekee, lakini CAF watakuwa makini kwani wanatambua vitendo visivyo vya kiungwana. Ni lazima tuwe makini na kuonyesha tumejifunza na tumebadilika," amesema Ally.