CAF yamfungia mechi 8 Kocha wa Taifa Stars, huku TFF ikimsimamisha. Aliishutumu Morocco kwa kupanga mechi

CAF yamfungia mechi 8 Kocha wa Taifa Stars, huku TFF ikimsimamisha. Aliishutumu Morocco kwa kupanga mechi

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limemfungia mechi nane Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Adel Amrouche kwasababu ya shutuma zake alizozitoa dhidi ya Morocco

Adhabu hiyo ulitolewa jana na Kamati ya Nidhamu ya CAF baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (RMFF) ikimlalamikia Kocha huyo kwa kauli zake kuwa Morocco inaushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja na waamuzi.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemsimamisha Kocha Adel Amrouche

Kutokana na uamuzi huo na imemteua Hemed Morocco kuwa Kaimu Kocha Mkuu akisaidiwa na Juma Mgunda.

View attachment 2876717
CAF nayo inapenda kuzunguka badala ya kunyooka. Si waseme tu kuwa wameamua kuiondoa timu ya taifa ya Tanzania.
 
Yeye na TFF wamejaza wachezaji wa ligi daraja tatu ulaya ili mradi timu ionekane ina wachezaji kutoka ulaya halafu anaanza kulaumu wengine,nchi hii siasa zinaharibu kila sekta.
Miaka kibao timu hii ilikuwa na wachezaji wanaocheza hapahapa nyumbani,TULIFIKA WAPI?
hoja yako haina mashiko
 
Mpira anao piga Haji hauoni?
Huyo jamaa atakuwa na shida au hajui mpira hivi kwa mpira anaoupiga Haji Mnoga unataka akae nani anayeweza kucheza zaidi yake nchi hii
 
Kuzarau makocha wazawa itatucost sana Kocha hana uchungu hakuwa hata na malengo mazuri akapewa timu afu tunashangaa kwann west Africa & North Africa wanaongoza,,,bora asepe tu
 
Mkuu Tff wanakosa gani ? Chama cha mpira ni msimamizi wa mchezo wa mpira , jukumu la kutengeneza wachezaji ni jukumu la vilabu vya mpira, ukiangalia wachezaji wetu ni sawa na Kuku wa kienyeji hawajui kesho yao watakula nini na chakula watakipata wapi, tofauti na kuku wanaofugwa kitaalamu. Mchezaji anacheza Simba lakini haijulikani tokea utoto wake kakelewa Academy ipi.
Tff inawajibika kwa kuleta kocha na benchi la ufundi wenye uwezo.
Kingine kuna wachezaji mfano Benard Kamungo alikuja Tanzania lakini akapuuzwa akaamua kurudi kuchezea usa .

Kuna kinda aliyezaliwa Tanzania aliyenunuliwa na Bayern Munich tff walishindwa nini kutumia kila ushawishi achezee Tanzania?
Viongozi wamezubaa hawana ubunifu sio Kama mataifa mengine.

Ben Morrison Wameshindwa nini kumpatia uraia na ameomba muda mrefu .
Hawa mastaa wa yanga , simba ma azam ambao mataifa Yao Wameshindwa kuwadhamini wanashindwa nini kuwapa uraia?
Mpira una mbinu ndani na nje ya uwanja.
 
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limemfungia mechi nane Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Adel Amrouche kwasababu ya shutuma zake alizozitoa dhidi ya Morocco

Adhabu hiyo ulitolewa jana na Kamati ya Nidhamu ya CAF baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (RMFF) ikimlalamikia Kocha huyo kwa kauli zake kuwa Morocco inaushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja na waamuzi.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemsimamisha Kocha Adel Amrouche

Kutokana na uamuzi huo na imemteua Hemed Morocco kuwa Kaimu Kocha Mkuu akisaidiwa na Juma Mgunda.

View attachment 2876717
taarifa ya CAF rasmi IKO WAPI ,Hii ni ya TANZANIA FOOBALL FAILURE(TFF), AU ndio wanampakazia kwakuwa kakataa kupangiwa wachezaji? taarifa ya CAF KAMA mnayo iwekeni hadharani pia tujue. hapo watakuwa wamemuangushia jumba bovu maana kaingia kwenye 18 zao. bongo mpira bado sana
 
Kwa tulioangalia mechi kocha alikuwa sahihi, hao makocha wa ndani Wana mafanikio gani
Alikuwa sahihi. Motsepe aangalie maofsa wake wa chini. Wachezaji wa nchi za kiarabu wanafake sana kuchezewa faulo. Hata kama hawajaguswa wanatoka yowe la kudanganya marefa. Alafu ni wapotezaji wazuri wa muda timu zao zinapokiwa zinaongoza
 
Nilipoona nchi inawateua MWIJAKU NA BABA LEVO kwa ajili ya Ushindi wa Taifa Star nikasema ngoja tuone. Nilifikiri waziri wa michezo angeteua ma legendary halisi wa soka kwenda kuongeza moja mbili tatu kwa vijana wetu hata nje ya uwanja. Hata kama legends wetu hawakucheza ulaya na hawakufika Afcon lakini wana kitu kikubwa kiushauri na hamasa kuliko hawa wasanii wa vichekesho na uchawa. Wapo kina Lunyamila, Julio, Mwameja, Mkwasa, Kibadeni, Pawasa nk. Na legends wapya kama John Boko, Kanavaro, Kaseja, Manyika, Erasto Nyoni
 
Alikuwa sahihi. Motsepe aangalie maofsa wake wa chini. Wachezaji wa nchi za kiarabu wanafake sana kuchezewa faulo. Hata kama hawajaguswa wanatoka yowe la kudanganya marefa. Alafu ni wapotezaji wazuri wa muda timu zao zinapokiwa zinaongoza
Kuna mchezaji mmoja wa Tanzania alichezewa rafu Mara tatu mfululizo na yule kiungo was man u Tena alikuwa na Kadi ya njano lakini hakufanya kitu
 
M
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limemfungia mechi nane Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Adel Amrouche kwasababu ya shutuma zake alizozitoa dhidi ya Morocco

Adhabu hiyo ulitolewa jana na Kamati ya Nidhamu ya CAF baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (RMFF) ikimlalamikia Kocha huyo kwa kauli zake kuwa Morocco inaushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja na waamuzi.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemsimamisha Kocha Adel Amrouche

Kutokana na uamuzi huo na imemteua Hemed Morocco kuwa Kaimu Kocha Mkuu akisaidiwa na Juma Mgunda.

View attachment 2876717
Morocco na Juma Mgunda tena? Dah hii kali
 
Back
Top Bottom