CAF yamtaja afisa usalama mechi ya Simba Vs AS Vita

CAF yamtaja afisa usalama mechi ya Simba Vs AS Vita

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Inspekta Hashimu Abdallah kuwa Ofisa Usalama wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) kati ya Simba SC na AS Vita Club FC (DR Congo) utakaochezwa Aprili 3, 2021 saa 10;00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Tanzania

tanfootball_1640903265251467318403516549396938767464012n.jpeg

Simba inayoongoza kundi A kwakuwa na alama 10 nyuma ya Al Ahly wenye pointi 7 na AS Vita wenye alama 4 mpaka sasa huku AL Merreikh ikiburuza mkia kwa kuwa na ponti moja pekee.

simbasctanzania_14884391937405419093674516550002000190214641n.jpeg

Wawakilishi hao wa Tanzania watatakiwa kushinda mchezo huu wa nyumbani dhidi ya AS Vita ili kujihakikisha nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Mabingwa Afrika.

simbasctanzania_1490288584223739623512537425447678342469556n.jpeg

Kwenye mchezo wa kwanza waliyokutana nchini Congo, Simba ilifanikiwa kuondoka na pointi tatu baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja na la pekee dakika ya 60 kwa njia ya mkwaju wa penati na mchezaji wao Mugalu.
 
Kwa mujibu wa hesabu ,Hata simba afungwe mechi zote robo Fainali kashapita .
Hesabu za wapi?

AlAhaly point 7 baki mechi 2 akishinda ana kuwa na points 13
AS vita point 4 baki mechi 2 akishinda ana kuwa na points 10

Al ahaly vs simba
Simba vs as vita

Simba ana points 10 mechi zimebaki mbili zidi ya as Vita na al ahaly

Simba ana magoli matano ya kushinda nazani hajaruhusu goli...

Al ahaly ana goli 8 amefungwa 3 gd 5

As vita ana goli 6 amefungwa 7 gd -1

Simba kama ktk mechi mbili zilizo baki akiruhusu magoli zaidi ya mawili kwa kila mechi bila ya yeye kupata goli basi safari yake itaishia hapo

Endapo matokeo yatakuwa

Simba 0 v As vita 1

Al ahaly 3/2 v simba

As vita 3 v almerrek 0

As vita ana jikusanyia 6 points na magoli 4

Simba ana jikusanyia 0 points na magoli -3/-4

Tukienda tafuta GD kt ya As vita na Simba

Simba atakuwa na GD 1/2
As vita atakuwa na GD 3

Hivyo As vita bado ana nafasi...

Muhimu Simba ashinde mechi yake kuweka uhakika wa safari yake

Na ana weza maliza sawa na alahaly kwa 13 points au juu yake na hata chini yake kama ataweza kuwa na mkakati mzuri
 
Simba itampiga As Vita hapa kwa Mkapa,mechi ya mwisho Simba Vs Al Alhly atapigwa pia japokuwa pia inaweza kuwa draw.
 
Hesabu za wapi?

AlAhaly point 7 baki mechi 2 akishinda ana kuwa na points 13
AS vita point 4 baki mechi 2 akishinda ana kuwa na points 10

Al ahaly vs simba
Simba vs as vita

Simba ana points 10 mechi zimebaki mbili zidi ya as Vita na al ahaly

Simba ana magoli matano ya kushinda nazani hajaruhusu goli...

Al ahaly ana goli 8 amefungwa 3 gd 5

As vita ana goli 6 amefungwa 7 gd -1

Simba kama ktk mechi mbili zilizo baki akiruhusu magoli zaidi ya mawili kwa kila mechi bila ya yeye kupata goli basi safari yake itaishia hapo

Endapo matokeo yatakuwa
Goal
Simba 0 v As vita 1

Al ahaly 3/2 v simba

As vita 3 v almerrek 0

As vita ana jikusanyia 6 points na magoli 4

Simba ana jikusanyia 0 points na magoli -3/-4

Tukienda tafuta GD kt ya As vita na Simba

Simba atakuwa na GD 1/2
As vita atakuwa na GD 3

Hivyo As vita bado ana nafasi...

Muhimu Simba ashinde mechi yake kuweka uhakika wa safari yake

Na ana weza maliza sawa na alahaly kwa 13 points au juu yake na hata chini yake kama ataweza kuwa na mkakati mzuri
Goal difference si kipaumbele sana katika mashindano haya, endapo timu zinamaliza na point sawa, kinachoangaliwa kwanza ni head to head kwa timu zilizofungana point kwa mfumo wa home and away Kama ilivyokuwa katika hatua ya mtoano, hivyo basi endapo Simba itamaliza na point 10 na Vita point 10, kitakacho angaliwa kwanza ni matokeo ya jumla ya mechi zao 2, lakini endapo Vita itaifunga Simba 1 bila hiyo matokeo ya jumla Kati ya Simba na Vita yatakuwa sare ya 1-1 ni hapo basi Sheria ya goal difference ita apply
 
Back
Top Bottom