Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 24,606
- 39,289
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Inspekta Hashimu Abdallah kuwa Ofisa Usalama wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) kati ya Simba SC na AS Vita Club FC (DR Congo) utakaochezwa Aprili 3, 2021 saa 10;00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Tanzania
Simba inayoongoza kundi A kwakuwa na alama 10 nyuma ya Al Ahly wenye pointi 7 na AS Vita wenye alama 4 mpaka sasa huku AL Merreikh ikiburuza mkia kwa kuwa na ponti moja pekee.
Wawakilishi hao wa Tanzania watatakiwa kushinda mchezo huu wa nyumbani dhidi ya AS Vita ili kujihakikisha nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Mabingwa Afrika.
Kwenye mchezo wa kwanza waliyokutana nchini Congo, Simba ilifanikiwa kuondoka na pointi tatu baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja na la pekee dakika ya 60 kwa njia ya mkwaju wa penati na mchezaji wao Mugalu.